img

Mbunge Amida ” aivalia kibwebwe changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa

December 9, 2020

Na Ahmad Mmow, Lindi.

Mbunge wa jimbo la Lindi, Amida Abdallah ( CCM) amesema kwa kushirikiana na wadau wa elimu na maendeleo ataendelea kujitolea kutatua changamoto ya vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari zilizopo katika jimbo hilo.

Mbunge Amida ametoa ahadi hiyo leo alipozungumza na walimu wa shule ya sekondari ya Ngongo baada ya kutembelea shule hiyo iliyopo katika manispaa ya Lindi.

Mheshimiwa Amida ambaye ameahidi kutoa mifuko 100 ya saruji itayotumika kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule hiyo, alisema lengo lake nikuona wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri na rafiki ambayo yatawafanya wasome kwa furaha.

Alisema katika baadhi ya shule majengo nimabovu yanayo hitaji ukarabati. Huku mengine ujenzi wake ukiwa umesimama kwa muda mrefu na kusababisha uhaba wa vyumba vya madarasa. Hivyo kusababisha wanafunzi kusoma katika mazingira yasiyofaa.

” Nilikwenda pia Mitwelo nimeikuta changamoto ya madarasa, nako nimeahidi kupeleka mifuko ya 100 ya saruji. Naahidi nitatekeleza yangu haraka. Baadhi ya shule hata vyoo vimechoka, nilazima tutae changamoto hizi,” Amida Alisema.

Hata hiyo alitoa wito kwa wazazi kuchangia ujenzi wa miundo mbinu ya shule. Ikiwamo vyumba vya madarasa na vyoo badala ya kutegemea serikali ambayo inamambo na miradi mingi inayotekeleza na kushughulikia. Huku pia akitoa wito kwa madiwani kushiriki kikamilifu katika kutatua changamoto hiyo. Ikiwamo kuhamasisha wananchi washiriki kikamilifu katika zoezi hilo.

” Naomba mniambie changamoto zenu kama Mbunge wenu, zile ninazo weza kuzitatua nitatue. Zile ambazo zinahitaji kupelekwa na kufikishwa katika mamlaka nitafikisha na kusukuma ili zitatuliwe,” Alisisitiza Mbunge Amida.

Aidha Mbunge huyo  aliwatia moyo walimu kwakuwaomba waendelee kufanyakazi kwa juhudi na maarifa licha ya changamoto ndogo ndogo wanazo kutananazo. Kwani serikali inatambua na kuthamini kazi kubwa wanayofanya. Kwahiyo itaendelea kushughulikia changamoto hizo hatua kwa hatua kadiri itakavyowezekana.

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo yenye wanafunzi 450, Alphonce Ngajiro alisema shule hiyo ina vyumba nane vya madarasa kati ya vyumba kumi vinavyohitajika. Huku akibainisha kwamba vyumba viwili vinajengwa. Kwahiyo baada ya kukamilika ujenzi wa vyumba hivyo, itakuwa na vyumba kumi vinavyohitajika.

Alizitaja baadhi ya changamoto katika shule hiyo kuwa ni umeme,maji, barabara ya kutoka barabara kuu kwenda shuleni hapo. Huku akitoa wito kwa wazazi wajenge utamaduni wa kuwalaza watoto wao kwenye mabweni yaliyopo shuleni hapo badala ya majumbani kwao.

Alisema wanafunzi wanaolala bwenini nirahisi kudhitibiwa kuliko wanaolala majumbani. Kwahiyo ni vema wazazi watambue umuhimu na faida ya  watoto kulala bwenini na madhara ya kulala nyumbani.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *