img

Mataifa yamechelewa kuwasilisha ripoti kuhusu hali ya hewa-UN

December 9, 2020

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wiki iliopita alihimiza umuhimu wa kulinda hali ya hewa akisema wanadamu wako kwenye hatari ya kuangamiza mazingira.

Kwenye mkataba wa Paris uliotiwa saini 2015, mataifa yalikubaliana kudumisha viwango vya joto chini ya nyusi 2 Celcius, wakati shirika la Umoja wa Mataifa la UNDP, likisaidia mataifa 115 kati ya 197 yaliotia saini mkataba huo kuhakikisha kuwa hali ya heya inadhibitwa, mengi yakiwa maskini.

Mataifa hayo yanachangia karibu robo moja ya gesi inayotokana na greenhouse ulimwenguni yakiwemo Mexico na Nigeria. UNDP hata hivyo limesema kuwa huenda janga la Covid-19 likawa kizingiti cha mataifa mengi kuwasilisha ripoti zao kwa wakati.

Kufikia sasa, ni mataifa 8 pekee yalioko chini ya program ya UNDP, ambayo yamewasilisha ripoti zao yakiwemo Rwanda na Mongolia.

-Imetayarishwa na Harrison Kamau, VOA Washington DC.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *