img

Mahakama ya juu Marekani yakataa kubatilisha ushindi wa Biden Pennsylvania

December 9, 2020

 

Rais wa Marekani Donald Trump amepata pigo jingine katika juhudi zake za kutaka ushindi wa rais mteule Joe Biden ubatilishwe, baada ya mahakama ya juu nchini humo kukataa ombi la wapambe wake kutaka matokeo ya uchaguzi katika jimbo la Pennsylvania yasiidhinishwe.

Mahakama hiyo iliyo na majaji watatu walioteuliwa na Trump miongoni mwa majaji tisa, haikutoa maelezo kuhusu uamuzi wake, na hakuna hata jaji mmoja aliyekuwa na uamuzi tofauti na wa wengine. 

Kwa zaidi ya mwezi mmoja tangu uchaguzi wa Novemba 3, Trump anaendelea kutoa madai kwamba kulikuwa na visa vya udanganyifu lakini bila ya ushahidi, na ameendelea kukataa kukubali kushindwa na Mdemocrat Joe Biden ambaye anaongoza kwa kura milioni saba dhidi yake. 

Trump na wapambe wake wamewasilisha kesi kadhaa mahakamani katika baadhi ya majimbo, lakini nyingi ya kesi hizo zimetupwa nje.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *