img

JPM akerwa na Mkurugenzi aliyenunua gari Mil 400

December 9, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amemtaka Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo kumwondoa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Geita kutokana na matumizi mabaya ya pesa.

”Hapo nataka kusema ukweli tuelewane hili la matumizi mabaya. Unakuta mkurugenzi ananunua gari la milioni 400 fedha tumehangaika nazo kuzipata wananchi, watoto wanachangishwa unakuta madawa hayatoshi. Nataka  kazi yako ya kwanza kwenda kumsimamisha mkurugenzi wa Geita ndio kazi yako ya kwanza ukaanze nayo” – Dkt. Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amemtaka Waziri Jafo kusimamia vizuri matumizi ya pesa kwenye Wizara hiyo kwasababu ndio changamoto kubwa iliyoonekana na ilimfanya afikirie sana kumrejesha kwenye nafasi yake.

“Tamisemi kuna matumizi mabaya ya fedha Jafo (Suleiman- Waziri wa Tamisemi) umefanya vizuri sana lakini kwenye kudhibiti fedha bado, nimefikiria sana kukurudisha au kutokukurudisha”, amesema Magufuli.

Baraza la Mawaziri limeapishwa leo Desemba 9, 2020, ambapo jumla ya Mawaziri 22 na Manaibu Mawaziri 23 wameapishwa katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Dodoma.

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *