img

IS ‘ilijaribu kutengeneza ndege zisizo na rubani zenye injini ya jet’, ripoti imeeleza

December 9, 2020

Dakika 5 zilizopita

Injini iliyotengenezwa na IS

Wanamgambo wa Islamic State (IS) lilijaribu kutengeneza ndege zisizo na rubani zenye kasi, zinazotumia nguvu ya injini ya jet kama zile zilizotumiwa katika mabomu ya V-1 yaliyodondoshwa Uingereza wakati wa vita ya pili ya dunia , uchunguzi umebaini.

Waangalizi wa masuala ya mizozo , Conflict Armament Research (CAR) wamebainisha injini kwenye ripoti mpya kuhusu namna gani IS ilipata na kutengeneza silaha

Tangu mwaka 2014, IS iliweka utawala wake wa kikatili kwa mamilioni ya watu, walipodhibiti eneo la kilomita za mraba 88,000 la mamlaka linaloanzia Magharibi mwa Syria kuelekea Mashariki mwa Iraq.

IS walitangazwa kudhibiwa nchini Syria na Iraq mwezi Machi mwaka 2019.

Baada ya miaka mitano ya mapambano makali, vikosi vinavyoungwa mkono na Marekani na washirika wake waliweza kurejesha maeneo yaliyokuwa yakidhibitiwa na IS.

“Hakuna kundi jingine lolote lenye silaha linalofikia uwezo na uzalishaji wa silaha wa IS,” Mike Lewis, Mkuu wa taasisi ya CAR aliyoongoza uchunguzi huo ameeleza.

Namir Shabibi, Mkuu wa shirika la operesheni nchini Iraq, amesema “wanamgambo waliobaki Iraq na Syria wamekuwa machachari katika kipindi cha mwaka uliopita”.

Ripoti ilibaini nini ?

Ripoti ya CAR, iliyotolewa Jumanne, ilikuwa ni matokeo ya uchunguzi wa miezi 18 kuhusu mitandao ya ununuzi na utengenezaji wa silaha za IS.

Ripoti hiyo ilisema uzalishaji “ulizidi kuimarika kiufundi na ulioboreshwa sana kati ya mwaka 2014 na 2017, urefu wa kile kinachoitwa ukhalifa wa IS.

Ripoti hiyo ilisema vifaa muhimu vilivyotumiwa na vikosi vya IS huko Iraq na Syria kutengeneza silaha na vilipuzi vilitokana ununuzi mkubwa uliofanywa na biashara zinazoendeshwa na familia huko Ulaya na Uturuki.

Mwanajeshi wa kikosi maalumu Iraq akifyatulia risadsi ndege isiyo na rubani iliyorushwa na Wanamgambo wa IS mwaka 2017

Manunuzi makubwa yaliyofanywa mwaka 2014 na mwaka 2015 ziliendelea kusukuma ongezeko za uzalishaji wa silaha wa IS mpaka walipopoteza udhibiti mwaka 2019. Ripoti ilieleza.

“Idadi ndogo ya watu muhimu na wafanya biashara walikuwa kitovu cha shughuli za ugavi wa bidhaa kuanzia za masuala ya uchunguzi, hadi mbolea kwa ajili ya kutengeneza vilipuzi,”Bwana Lewis alisema

“Lakini biashara hii inaweza kuwa imevurugwa.”

Ripoti hiyo ilisema matumizi ya IS ya ndege zisizo na rubani yalilenga sana ndege ndogo, zinazotumia umeme, ambazo zinapatikana kibiashara ulimwenguni.

Vikoi vya Peshmerga vikikusanya vifaa vya chombo cha anga (UAV)

Lakini uchunguzi ulibaini kuwa, kuanzia mwaka 2015 na kuendelea, wataalamu wa IS ” pia walitazamia kutengeneza, chombo cha anga (UAVs) kinachoendeshwa na nguvu ya injini ya Jeti”.

Ripoti hiyo ilisema “injini ya ndege iliyojengwa kikamilifu” yenye urefu wa zaidi ya mita mbili ilipatikana katika hospitali iliyoko Magharibi mwa Mosul, Iraq mnamo Septemba 2017.

Injini hizo zilitengenezwa kwa ajili ya kipindi cha vita vya pili vya dunia V-1 ‘makombora yanayosafiri,” ripoti ilisema.

Makombora ya V-1 yalitumiwa na jeshi la Nazi la Ujerumani wakati wa Vita vya pili vya dunia. Injini za ndege aina ya Pulse “ziliacha kutumika kwa ndege kamili mnamo miaka ya 1950”, lakini imebaki kuwa “ya bei rahisi”, ilisema ripoti hiyo.

Wachunguzi walisema mfumo wa kujiendesha wa kupambana na ndege ulikuwa mmoja wa “mifumo mipya ya silaha” iliyotengenezwa na kujaribiwa lakini haikutumika.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *