img

Fedha zilizopangwa kutumika katika sherehe za Uhuru kutumika kununua vifaa katika hospitali ya Uhuru Dodoma

December 9, 2020

Watanzania leo wanaadhimisha miaka 59 ya Uhuru wa Tanganyika.

Kwa mwaka huu hakutakuwa na sherehe za Uhuru na badala yake fedha zilizopangwa kutumika katika sherehe hizo zitatumika kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya hospitali ya Uhuru iliyopo jijini Dodoma.

Fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hizo ni Shilingi Milioni 835.4.

Hospitali hiyo ya Uhuru ilianza kujengwa mwaka 2019 baada ya Rais John Magufuli kuagiza fedha zilizotengwa kwenye sherehe za Uhuru mwaka 2018  ambazo ni Shilingi Milioni 915 kuelekezwa katika ujenzi huo.

Serikali imewataka Watanzania wote kusherehekea sherehe za miaka 59 ya Uhuru wa Tanganyika kwa kufanya kazi za kijamii katika maeneo yao.

Tanganyika ilipata Uhuru wake Disemba 9 mwaka 1961.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *