img

Coronavirus Kenya: Daktari aliyewasaidia watoto kutabasamu

December 9, 2020

Dakika 3 zilizopita

Dkt Ashraf Emarah

Maelezo ya picha,

Dkt Emarah ambaye ni mzaliwa wa Misri, amefanya kazi Kenya kwa miongo kadhaa

Kifo cha Dkt Ashraf Emar, mtaalamu wa ngazi ya juu wa upasuaji wa kurekebisha viungo nchini Kenya kilichotokana na ugonjwa wa corona mwezi uliyopita, kiliangazia hali ya wataalamu wa afya ambao wanataka vifaa kinga wanapokabiliana na janga la corona, kama anavyo ripoti mwandishi wa BBC Basillioh Mutahi.

Wakati daktari huyo wa upasuaji na mtaalamu wa ngazi ya juu magharibi mwa Kenya aliambukizwa virusi vya corona na hali yake kuwa mbaya zaidi hapakuwa na kitanda cha kuwahudumia wagonjwa mahututi katika hospitali ya- Rufaa ya Moi mjini Eldoret.

Dkt Emarah aliwafunza aliwafunza wanafunzi wa chuo cha matibabu cha Eldoret, hospitali ya pili kuu ya rufaa nchini kwa miongo kadhaa.

Madaktari na familia yake walijaribu kumleta Nairobi mamia ya maili kutoka huko.

Lakini gharama ya kupata ambulensi na ndege ya kufikisha Nirobi ilikuwa “ghali sana”, afisa mmoja wa chama cha madaktari alisema. Dawa muhimu ambayo ingelimsaidia hali yake ilipokuwa mbaya pia ilikuwa vigumu kupata kutokana na bei yake ghali.

Dr Emarah was a lecturer of plastic Surgery at the Department of Surgery and Anaesthesiology, School of Medicine, Moi University

Maelezo ya picha,

Dkt Emarah aliwafanyia upasuaji watoto waliokuwa na matatizo ya mdomo

“Madaktari walilazimika kuchagishe fedha ili kununua dawa” ya kumsaidia, Dkt Chibanzi Mwachonda, kaimu katibu mkuu wa chama cha madaktari nchini Kenya (KMPDU), aliambia kamati ya bunge .

“Ilikuwa hali ya kusikitisha ,” Dkt Mwachonda alisema, akiongezea kuwa madaktari hawana bima kamili ya matibabu kutoka kwa bima ya kitaifa.

Daktari huyo mgonjwa alipelekwa katika hospitali ya kibinafsi ya Nakuru, mji ambao uko kati kati ya Eldoret na Nairobi, ambako alisubiri kupatikana kwa kitanda cha wagonjwa mahututi mjini Nairobi.

Lakini siku moja baadaye, Ijumaa ya Novemba 13, akafariki dunia.

Uhaba wa madaktari

Dkt Emarah alikuwa daktari mtaalamu wa nne kufariki wiki hiyo, katika nchi hiyo aliyo na karibu madktari 7,000 wanaohudumia watu milioni 48.

Wiki moja kbla ya kifo chake, alikuwa akifanya upasuaji na kusimamia wanafunzi,kabla aanze kupata dalili ya maambukizi siku kadhaa baadaye, rafiki yake Dkt Anthony Akoto aliambia BBC.

“Alifariki akiwa kazini,”alisema Dkt Akoto, ambaye pia ni afisa wa chama cha madaktari, akiongeza kuwa kifo kumemchukua daktari pekee wa upasuaji wa kurekebisha viungo aliyekuwa na tajiriba kubwa magharibi mwa Kenya.

“Nchi ina daktari wachache wa upasuaji wa aina hiyo. Katika kitengo chake, alikuwa peke yake, japo kuna wengine wanainukia, bado ameacha pengo.”

Bodi ya wahudumu wa afya nchini Kenya iliwaorodhesha wataalamu wanne peke wa upasuaji wa kurekebisha viungo nchini kufikia mwaka 2018.

Dkt Emarah ambaye ni mzaliwa wa Misri, aliwasili nchini Kenya karibu miaka 30 iliyopita, ameelezewa na wafanyakazi wenzake kuwa mwalimu na mjuzi ambaye atakumbukwa na wengi.

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya video,

Virusi vya Corona: Mapambano ya kuthibisha uwepo wa Covid-19

Daktari huyo alijulikana sana kutokana na upasuaji wa kurekebisha midomo ya watoto waliozaliwa wakiwa na mmpasiko na kuwasaidia kutabasamu. Alitoa mafunzo kwa wanafuzi wanaosomea upasuaji wa aina hiyo hata kwa nchi jirani kama vile Somalia, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

“Tunamuomboleza rafiki na mshirika wetu,” Smile Train Africa, moja ya mashirika ya kutoa misaada ilisema, na kuweka picha ya daktari huyo katika mtandao wa Twitter akiwa na baadhi ya watoto aliowafanyia upasuaji.

“Tunatuma rambi rambi zetu kwamke na watoto wake, marafiki, wafanyakazi wenzake, na wagonjwa aliowahudumia wakati wa uhai wake pamoja na madaktari wa upasuaji aliowapa mafunzo na ambao wataendeleza taaluma yake.”

Coronavirus street art

Maelezo ya picha,

Viwango vya maambukizi ya kila siku ya virusi vimeongezeka nchini Kenya

Tangu virusi vya corona vilipogunduliwa nchini Kenya mwezi Machi mwaka 2020, karibu madaktari 14 wamefariki kutokana na janga hilo

Siku ya Jumatatu chama cha madaktari KMPDU, kilitangaza kifo cha Dkt Stephen Mogusu ambaye alifariki kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Kando na madkatari hao, karibu wauguzi 20 na maofisa 10 wa matibabu wamefariki kutokana na virusi hivyo.

2px presentational grey line

Maelezo zaidi kuhusu corona Kenya:

2px presentational grey line

Kwa ujumla karibu wahudumu wa afya 2,000 wameambukizwa virusi vya corona, miongoni mwao Dkt Mwachonda, afisa wa ngazi ya juu wa chama cha madaktari, ambaye hivi karibuni alielezea jinsi ilivyoathirika kiakili.

“Ulikuwa wakati mgumu sana kwangu mwaka huu… Kuna wakati nilikuwa nimekata tamaa – Nilihisi kana kwama : ‘Sitapona maradhi haya,’” aliambia kituo cha televisheni cha NTV.

Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona nchini Kenya imekuwa ikiongezeka tena katika wiki za hivi karibuni,mwezi Novemba ikirekodi idadi ya juu ya maambukizi ya kila siku pamoja na vifo tangu janga hilo lilipoanza nchini humo.

Nchi hiyo kufikia sasa imethibitisha kuwa watu zaidi ya 88,000 wameambukizwa virusi vya corona, ikiwemo vifo 1,500.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *