img

Boris Johnson asema bado kuna uwezekano wa kuwa na mkataba mzuri na EU

December 9, 2020

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, amesema leo kwamba bado kuna uwezekano wa kufikia mkataba wa kibiashara baada ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Johnson ameyasema hayo bungeni Uingereza kabla ya kuanza safari kuelekea Brussels Ubelgiji, kwa mazungumzo na rais wa kamisheni kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen.Ameliambia bunge kuwa bado kunapaswa kuwa na makubaliano mazuri na kwamba anatarajia kuzungumza zaidi na von der Leyen kuhusu hilo usiku wa leo.

Katika tukio jingine mapema leo, kansela wa Ujerumani Angela Merkel pia alisema bado anaona kuna nafasi ya makubaliano baada ya Uingereza kuondoka kikamilifu katika umoja huo.Lakini ameonya kwamba Umoja wa Ulaya utapinga kile alichokitaja kuwa “masharti yasiyokubalika”.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *