img

Watu 68 wapoteza maisha kwenye mafuriko

December 8, 2020

Watu 68 wameripotiwa kupoteza maisha kwenye mafuriko yaliyosababishwa na mvua nyingi zilizonyesha nchini Nigeria.

Msimamizi wa Shirika la Dharura la Kitaifa la Nigeria (NEMA) Muhammadu Muhammed, alitoa taarifa na kusema kuwa, mikoa 320 tofauti ya majimbo 35 ikiwemo mji mkuu wa Abuja, imeathirika kwa mafuriko ndani ya mwaka huu.

Muhammed alibaini kuwa zaidi ya watu 129,000 pia waliathirika kwa maafa ya mafuriko ambapo 68 walipoteza maisha.

Akifahamisha kuwa mafuriko hayo pia yamesababisha ukosefu wa chakula, Muhammed alisema,

“Mbali na kupoteza maisha, maelfu ya nyumba pia ziliharibiwa na ardhi ya mashamba kuathirika kutokana na mafuriko. Hii imekuwa na athari mbaya kwa usalama wa chakula.”

Mohammed aliongezea kusema kuwa NEMA imeazimia kutoa msaada kwa wakala wa dharura ili kuboresha uwezo wao wa kukabiliana na majanga.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *