img

Ujerumani imeteoa ridhaa kufanyika uchuguzi wa ubaguzi wa rangi kwa polisi

December 8, 2020

Baada ya mkwamo wa muda mrefu wa kisiasa, afisa wa juu kabisa wa Ujerumani mwenye dhamana ya usalama, ameamuru kufanyika utafiti kuhusu majukumu ya polisi, ambao utajumuisha uchunguzi wa kiwango cha ubaguzi wa rangi katika jeshi hilo. 

Wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani imesema utafiti huo, utafanyika kwa zaidi ya miaka mitatu, ikimaanisha matokeo yake yatapatikana wakati wa serikali ijayo ya Ujerumani, ambayo itakuwa na dhamana ya nini kifanyike kwa kile kitakachobainishwa. Wizara hiyo imesema utafiti unatafanya na Chuo Kikuu cha Polisi cha Ujerumani. 

Awali wizara ya mambo ya ndani inayoendeshwa kihafidhina, yenye kusimamia mwenendo wa poilisi ilikubali hatua hiyo lakini, baadaye ikabadili msimamo. Mjadala kuhusu ubaguzi wa kimfumo nchini Ujerumani uliongezeka, jambo ambalo lilichochewa zaidi na maandamano ya duniani kote na hasa baada ya kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *