img

Uganda yatuma maombi ya chanjo ya corona

December 8, 2020

Uganda imewasilisha ombi la kupata chanjo ya covid19 kama inavyotakiwa na COVAX facility, wizara ya afya ya Uganda imethibitisha kuwasilisha ombi hilo.

Ombi hilo limetumwa wakati maambukizi ya virusi vya corona nchini Uganda yakizidi kupanda kwa kasi huku baadhi ya wanasiasa wakituhumiwa kusambaza virusi vya corona kutokana na muingiliano wa watu katika kampeni.

Maneja wa mipango ya taifa ya upanuzi wa chanjo katika wizara ya afya nchini humo bwana Alfred Driwale ameiambia BBC kuwa wameanza mchakato huo kwa majuma mawili na sasa wamekamilisha na wamewasilisha jana jioni kwa COVAX Facility:

“Uganda ikiwa moja ya mataifa ya uchumi wa chini yanayokwenda kunufaika kutoka kwa COVAX Facility. Kufikia sasa hakuna chanjo iliochaguliwa kutumiwa katika mataifa,isipokuwa kuna maendeleo na matarajio ya majaribio ya chanjo ya corona kila siku kwa wanachama wa COVAX Facility. Hivyo mara chanjo itakapopatikana itakuwa rahisi kusambaza kwa mataifa yenye mahitaji”.

Dk.Driwale ameongeza kwamba chanjo hiyo itapewa watu waliomstari wa mbele katika kupambana na virusi vya corona pamoja na watu walio hatarini kuambukizwa virusi vya covid19 :

Kwa mujibu wa Shirika la afya duniani WHO, COVAX tayari imeshirikisha mataifa 186 duniani kati hayo 47 ni kutoka bara la Afrika.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *