img

Roma Mkatoliki atangaza kuacha Muziki

December 8, 2020

Msanii wa HipHop Roma Mkatoliki ameachia ujumbe wenye utata kwenye mtandao wake wa Instagram na Twitter, ambao unasema wimbo atakaoutoa safari hii ndiyo utakuwa wa mwisho kwake.

Roma ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani, kupitia ujumbe wake huo ameandika kuwa 

“Wimbo wangu wa kwanza niliutoa mwaka 2007, wimbo wangu wa mwisho nitatutoa muda wowote kuanzia sasa, na huu ndiyo utakuwa wimbo wangu wa mwisho, ahsanteni kwa kuni-support kwa kipindi chote cha miaka 13 nilichowadumia kwenye sanaa hii ya muziki”.

Taarifa hiyo inakuwa ya tatu kwa mwaka huu kwa wasanii wa muziki wa BongoFleva kutangaza kuacha muziki ambapo wa kwanza alikuwa ni Vanessa Mdee, Jolie na sasa ni Roma Mkatoliki.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *