img

Rekodi hatari za Mourinho na Kane dhidi ya Arsenal

December 8, 2020

 

Jose Mourinho ameendelea kuwa na rekodi bora dhidi ya Arsenal akiwa katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Arsenal, baada ya kukiongoza kikosi cha Tottenham kuibuka na ushidi wa mabao 2-0 dhidi ya majairani zao hao. Harry Kane amekuwa mfungaji bora wa muda wa dabi ya Kaskazini mwa London.

Mabao ya Spurs katika ushindi huo wa 2-0 yalifungwa na Son Heung-Min na Harry Kane, na ushindi huu umeifanya Spurs kuendelea kuongoza katika msimamo wa EPL wakiwa na alama 24 sawa na Liverpool walio nafasi ya pili.

Hizi ni baadhi ya rekodi za Jose Mourinho na Harry Kane baada ya ushindi dhidi ya Arsenal.

Kocha Jose Mourinho huu ulikuwa ni mchezo wake wa 11 anacheza dhidi ya Arsenal, akiwa kwenye uwanja wa nyumbani pasipo kupoteza, ushindi wa jana ulikuwa ni wa 7 huku pia akiwa amepata sare kwenye michezo 4.

Pia Mourinho amekuwa kocha wa pili kwenye historia ya Tottenham kushinda michezo yote miwili ya awali dhidi ya Arsenal baada ya ushindi wa jana, mchezo wake wa kwanza alishinda 2-1 mwezi julai mwaka huu, na kocha wa kwanza kufanya hivyo alikuwa Jimmy Anderson msimu wa 1955/56.

Harry Kane amekuwa kinara wa ufungaji kwenye dabi ya Kaskazini mwa Londoni amefikisha mabao 11, akiwaacha Emmanuel Adebayor, ambaye amechezea timu zote mbili (Arsenal na Spurs) na Bobby Smith ambao wana mabao 10 kila mmoja.

Kane amefikisha mabao 250 kwenye maisha yake ya soka, mabao 202 amefuka kwenye klabu yake ya sasa Spurs na mabao 32 amefunga akiwa na timu ya taifa ya England, 9 akiwa na Millwall, 5 na Leyton Orient na 2 akiwa na Leicester City.

Mshambulijai huyu wa England mwenye umri wa miaka 27, amepiga pasi za usaidizi wa magaoli (assists) 10 kwenye michezo 11 ya EPL msimu huu na akiwa kinara, ikiwa ni sawa na rekodi ya Mesut Ozil ya kupiga pasi hizo nyingi kwenye michezo michache ya mwanzo mwa msimu.

Pacha ya ushambuliaji ya Tottenham ya Harry Kane na Son Heung-Min inashika nafasi ya pili kwenye historia ya ligi kuu England kuwa imezalisha mabao mengi, wametengenezeana mabao 31, wakiwa nyuma ya pacha ya Frank Lampard na Didier Drogba ambao walitengenezeana mabao 36 wakiwa na kikosi cha Chelsea.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *