img

Mohsen Fakhrizadeh: Silaha yenye intelijensia ilitumika dhidi ya mwanasayansi wa Iran

December 8, 2020

Saa 2 zilizopita

Wanajeshi wa Iran wakiwa wamebeba jeneza la Mohsen Fakhrizadeh

Bunduki-ya setilaiti na “yenye intelijensia bandia” ilitumika kumuua mwanasayansi mkuu wa nyuklia wa Iran, kamanda wa jeshi la Iran ameeleza.

Mohsen Fakhrizadeh aliuawa kwa kupigwa risasi katika msafara nje ya Tehran tarehe 27 mwezi Novemba.

Brigedia Jenerali Ali Fadavi aliwaambia wanahabari wa eneo hilo kuwa silaha hiyo iliyokuwa imewekwa kwenye lori la kubeba mizigo, iliweza kufyatua risasi huko Fakhrizadeh bila kumpiga mkewe pembeni yake. Madai hayo hayakuthibitishwa.

Iran imeilaumu Israeli na kundi la upinzani lililohamishwa kwa shambulio hilo.

Israel haijakiri wala kukana kuhusika na mashambulizi.

Fakhrizadeh aliuawa vipi?

Mamlaka ya Iran imetoa madai ya kukanganya jinsi mwanasayansi huyo alivyopigwa risasi aliposafiri kwa gari kupitia mji wa Absard.

Siku ya shambulio hilo, wizara ya ulinzi ilisema kulikuwa na mapigano ya risasi kati ya walinzi wa Fakhrizadeh na watu kadhaa wenye silaha.

Ramani inayoonesha eneo alipouawa Mohsen Fakhrizadeh

Ripoti moja ya Iran iliwanukuu mashahidi wakisema kwamba “watu watatu hadi wanne, ambao wanasemekana walikuwa magaidi, waliuawa”. Gari aina ya Pick-up Nissan pia ilisemekana kulipuka katika eneo la tukio.

Katika hotuba kwenye mazishi ya Fakhrizadeh, mkuu wa Baraza Kuu la Usalama la Kitaifa la Iran alisema kwa kweli lilikuwa shambulio la mbali, kwa kutumia “njia maalum” na “vifaa vya elektroniki”. Lakini hakutoa maelezo zaidi.

Jenerali Fadavi, naibu kamanda wa jeshi la Iran , alisema huko Tehran siku ya Jumapili kwamba bunduki iliyowekwa kwenye gari la Nissan ilikuwa “na mfumo wa satelaiti ambao ulimlenga Fakhrizadeh” na “ilikuwa ikitumia intelijensia bandia”.

Risasi 13 zilipigwa kuelekea kwenye gari alilokuwa Mohsen Fakhrizadeh

Bunduki aina ya machine-gun “ililenga tu usoni mwa sFakhrizadeh kwa njia ambayo mkewe, licha ya kuwa umbali wa sentimita 25 tu, hakupigwa risasi”, alisema.

Jenerali huyo alisisitiza kwamba hakuna mshambuliaji yeyote aliyekuwa katika eneo la tukio, akisema kwamba “jumla ya risasi 13 zilifyatuliwa na zote zilipigwa kutoka kwenye [silaha] hiyo katika Nissan”. Risasi nne zilimpata Fakhrizadeh kichwani “wakati akijitupa”, aliongeza.

Kiongozi wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameapa kulipiza kisasi mauaji hayo, akidai “adhabu ya uhakika” ya waliotekeleza mauaji hayo.

Ijumaa, redio ya Umma ya Israel iliripoti kwamba maafisa wa usalama wa Israel walikuwa wameonya baadhi ya wanasayansi wa zamani wa nyuklia kuwa waangalifu. Wataalam walikuwa wakifanya kazi kwenye mtambo huko Dimona, eneo la siri la nyuklia katika jangwa la Negev.

Serikali ya Israel haikusema chochote ripoti hiyo, ambayo ilikuja siku moja baada ya wizara ya mambo ya nje ya Israel kuwaambia raia wa Israeli wanaosafiri Mashariki ya Kati na Afrika kuwa macho kulingana na kile ilichokiita vitisho kutoka kwa Iran.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *