img

Mgawanyo wa viti vya bunge Venezuela

December 8, 2020

 

Mgawanyo wa viti bungeni umetangazwa baada ya chama cha muungano wa serikali cha Grand Patriotic Pole (Gran Polo Patriotico) kinachoongozwa na Rais Nicolas Maduro kushinda uchaguzi wa bunge uliofanyika Venezuela siku ya Jumapili.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Venezuela Indira Alfonso, alitoa maelezo kwa waandishi wa habari na kutangaza kwamba asilimia 98.63 ya kura ilihesabiwa, na muungano ulioongozwa na chama tawala ulipata asilimia 68.43 ya kura na kushinda viti 177 kati ya viti 277 vya Bunge la Kitaifa (AN).

Akibaini idadi ya wapiga kura walioshiriki kwenye uchaguzi huo ilikuwa milioni 6,251,080, Alfonso alisema kuwa chama tawala kilikusanya kura milioni 4,277,926.

Alfonso pia alisema kuwa idadi ya waliojitokeza ni asilimia 31, vyama vya upinzani vilishinda viti 97 katika bunge kupitia kura milioni 1,950,170 walizopata

Kwa upande mwingine, iliarifiwa kuwa waangalizi 200 wa kimataifa na wasimamizi 1600 wa kitaifa walihusika katika shughuli ya usimamizi wa uchaguzi huo.

Chama cha muungano kilichoongozwa na Rais Maduro, kilitangaziwa ushindi hapo jana katika uchaguzi wa Bunge la Kitaifa (AN) uliosusiwa na wanasiasa wa upinzani.

Maduro alitoa hotuba kwenye kituo cha televisheni na kusema,”Tulishinda viti vya Bunge la Kitaifa kwa kura nyingi za wananchi wa Venezuela. Bila shaka huu ni ushindi mkubwa kwa demokrasia.”

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *