img

Mbio za wazi Haydom Marathon kufanyika Desemba 12 Mbulu

December 8, 2020

Na John Walter-Manyara

Mashindano ya  riadha mbio za wazi kwa watu wote yanayoandaliwa kila mwaka na  Hospitali ya Kilutheri  maarufu kama Haydom Marathon, kufanyika mwishoni mwa wiki hii Haydom wilayani Mbulu mkoani Manyara.

Taarifa za Uhakika kutoka kwenye uongozi wa Hospitali hiyo, imeeleza kuwa Mashindano hayo yatafanyika Jumamosi mwishoni mwa  wiki hii Desemba 12,2020 katika eneo la Haydom kuanzia majira ya asubuhi  yakiongozwa na Kauli mbiu isemayo “ KIMBIA KUOKOA MAISHA “

Taarifa hiyo imeeleza kuwa maandalizi kuelekea katika mashindano hayo yanaendelea vizuri ambapo washiriki wote watapaswa kufanya usajili katika hospitali ya Kilutheri Haydom.

Aidha wafanyabiashara watakaohitahi kuweka duka au banda katika eneo la kuanza na kumaliza mbio watapaswa kulipia shilingi elfu kumi.

Washiriki watu wazima watalipa shilingi elfu kumi   (10,000) na watoto watalipa shilingi elfu mbili (2000) tu.

Kipindi cha nyuma kabla ya mlipuko wa Homa ya mapafu (Covid 19) Mashindano hayo yalikuwa yakihudhuriwa na nchi jirani.

Washiriki wa mbio watachuana katika kilomita 21, kilomita 10 na kilomita 2 pamoja na mbio za watoto wenye umri chini ya miaka 15 za mita 100.

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *