img

Lloyd Austin achaguliwa na Joe Biden kuongoza wizara ya ulinzi

December 8, 2020

Dakika 6 zilizopita

Gen Lloyd Austin. File photo

Maelezo ya picha,

Jenerali Lloyd Austin atahitaji idhini rasmi kutoka baraza la Congress kwasababu alistaafu chini ya miaka saba iliyopita.

Rais mteule wa Mararekani Joe Biden amemchagua Jenerali mstaafu Lloyd Austin kama waziri wake wa ulinzi, vyombo vya habari vya Mareknai vimeripoti.

Iwapo ataidhinishwa Austin mwenye umri wa miaka 67-ambaye alistaafu mwaka 2016 atakuwa ndiye Mmarekani wa kwanza mweusi kuwahi kuiongoza Pentagon.

Atahitaji idhini maalumu ya congress kwani miaka anahitaji kuwa amekaa miaka saba kati ya jukumu la awali na kuwa mkuu wa jeshi.

Bw Biden amekuwa akikabiliwa na miito ikiwa ni pamoja na ile inayotoka katika jamii za Wademoctrat weusi, Waasia na Walatino waqkimtaka awateua watu kutoka jamii hizo kuchukua nyadhifa za uwaziri.

Afisa wa zamani wa Pentagon Michèle Flournoy, ambaye angekuwa mwanamke wa kwanza kuchukua wadhifa huo, amekuwa akiangaliwa kama miongoni mwa watu watakaopewa kazi hiyo-pamoja na Jeh Johnson, msauri wa zamani wa Pentagon na Waziri wa zamani wa usalama wa ndani.

Jenerali Austin mwenye nyota nne alihudumu chini ya utawala wa Obama, akiongoza Kituo kikuu cha Marekani kinachotoa Amri kuu za kijeshi , ambacho wajibu wake ulikuwa ni pamoja ni kutoa miongozo kuhusu Mashariki ya Kati ,Asia ya Kati na sehemu ya Asia Kusini kati ya mwaka 2013 na 2016. Alikuwa ndiye mwanajeshi pekee aliyepanga mashambulio dhidi ya kundi la Islamic State katika nchi za Iraq na Syria.

Kabla ya hapo alikuwa naibu mkuu wa majeshi wa jeshi na Jenerali wa mwisho wa vikosi vya majeshi ya Marekani nchini. Katika miaka hii alifanya kazi kwa karibu na Bw Biden, ambaye alikuwa ni Makamu wa rais katika utawala wa Obama.

Jenerali Austinana sifa ya uongozi bora na kwa kuepuka macho ya umma, kutoa mahojiano kidogo kwa waandishi wa habari na kuchagua kukutoongea wazi kuhusu harakati za kijeshi.

Joe Biden (left) and Gen Lloyd Austin in Iraq in 2011

Maelezo ya picha,

Joe Biden na Gen Lloyd Austin – katika picha waliyopigwa pamoja hapa nchini Iraq mwaka 2011 – walifanya kazi kwa karibu wakati wa utawala wa Obama

Jenerali Austin wakati mmoja aliangaliwa kama mgombea ambaye hakufikiriwa kwanza lakini katika siku za hivi karibuni aliibuka kama mgombea wa kwanza na chaguo salama.

Lakini uteuzi wake unaweza kuibua ukosoaji kutoka kwa makundi yanayotaka mabadiliko kuhusiana na wadhifa wa Jenerali Austin katika miaka ya hivi karibuni kama mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa ulinzi Raytheon na wadhifa kutoka kwa wabunge katika Congress ambao wanataka Pentagon iongozwe na raia.

Idhini inayohitajika ya bunge la congress imekwishawahi kutolewa mara mbili tu, hivi karibuni ikitolewa kwa James Mattis, Jenerali wa vikosi vya wanamaji ambaye alihudumu kama Waziri wa kwanza wa Ulinzi wa Donald Trump.

Bw Biden na Jenerali Austin bado hajatoa kauli yoyote kuhusiana na uiteuzi wake. Rais mteule alimpatia wadhifa huo na Jenerali Austin alikubali katika ujumbe alioutuma Jumapili, zimesema ripoti.

Taarifa ya uteuzi umetokea kabla ya mkutano baina ya Bw Biden, Makamu wa rais-mteule Kamala Harris na makundi ya haki za kiraia Jumanne . Rev Al Sharpton, mwanaharakati wa haki za kiraia, alisema kuwa uamuazi huo ni “hatua kuelekea njia inayofaa lakini bado haujafika mwisho wa safari”.

Uamuzi huo unakuja wiki mbili baada ya Bw Bidenkuwatangaza wajumbe wengine wa ngazi ya juuwa timu yake ya usalama wa taifa.

Bw Biden alimshinda rais Mrepublican Trump katika uchaguzi wa tarehe 3 Novemba. Rais amendelea kukataa kukubali matokeo katika uchaguzi, akidai , bila ushahidi , kuwa kulikuwa na wizi mkubwa wa kura.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *