img

Je, Kesi za ICC na BBI zitamwathiri vipi Naibu Rais Ruto kisiasa?

December 8, 2020

  • Hezron Mogambi
  • Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Nairobi

Dakika 7 zilizopita

m

Habari kwamba afisa mwendesha mkuu wa mashtaka kwenye mahakama ya kimaitaifa ya Uhalifu (ICC) Fatou Bensouda ni kwamba mahakama hiyo yenye makao makuu yake ni huko Hague iko tayari kupokea habari mpya kuhusiana na kesi zinazowahusu Naibu Rais William Ruto na mwanahabari Joshua Sang ni pigo kubwa kwa siasa zake na kujitayarisha kwake kuwania Urais kwenye uchaguzi wa mwaka wa 2022.

Itakumbukwa kuwa Dkt. Ruto alikuwa miongoni mwa watu sita walioshtakiwa dhidi ya uhalifu wa kibinadaamu ambayo ni pamoja na mauaji, kuwahamisha kwa nguvu na kuwatesa watu baada ya uchaguzi ulioibua mvutano mkubwa mwishoni mwa mwezi wa Desemba mwaka 2007 na kupelekea vurugu zilizosambaa nchi nzima mapema mwaka 2008.

Ikumbukwe kwamba kesi dhidi ya Dkt Ruto na Sang zilitupiliwa mbali na mahakama hiyo kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha.

Aliyekuwa kiongozi wa Mashtaka wakati huo, Fatou Bensouda aliilaumu serikali ya Kenya kwa kukataa akushirikiana na mahakama hiyo na muingilio wa kisiasa.

Lakini mwendesha mashtaka Fatou Bensouda sasa anasema yuko tayari kupokea ushahidi mpya kutoka kwa serikali ama mtu yeyote.

Mashataka dhidi ya Paul Gicheru

Haya yanatokea huku wakili kutoka Kenya, Paul Gicheru akiwa ameshajisalimisha na kesi dhidi yake kuanza kwenye mahakama hiyo ya ICC.

Kuanza kwa kesi hiyo pamoja na uwezekano wa ushahidi mpya kuwasilishwa na kuanza kwa kesi dhidi ya Bwana Ruto na Bwana Sang kuhusu machafuko ya baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka wa 2008-2009 kumezua na kuanzisha mijadala na mdahalo mpya kuhusiana na kesi kwenye mahakama ya ICC zilizowahusu William Ruto na wengine mwaka wa 2010 pamoja na athari zake kwenye siasa za Kenya huku uchaguzi wa mwaka wa 2022 ukakaribia.

Hayo yote yalianza mnamo Novemba 2, wakati wakili Paul Gicheru kutoka Kenya alipojisalimisha kwa wakuu wa nchi huko Udachi baada ya kuwasili jijini Amsterdam akiandamana na mkewe.

Baadaye, wakili huyu alitwaliwa kwa mahakama ya ICC ambayo ilikuwa tayari imetoa amri ya kukamatwa kwake na Wakenya wengine wawili mnamo Machi, 2015.

Wakenya hawa wawili waalikuwa wanatakiwa na mahakama ya ICC kushtakiwa kwa tuhuma za kuwahonga mashahidi, kwa kutumia mbinu za chini kwa chini kuhakikisha kuwa ushahidi dhidi ya Rais Kenyatta na naibu wake William Ruto na mwanahabari Joshua Sang haufui dafu.

Kesi hizo za Wakenya ambazo mwanzoni zilikuwa sita, zote zilisitishwa kwa ukosefu wa ushahidi na mashahidi.

Kesi za ICC na kuchaguliwa kwa Uhuru na Ruto

m

Kesi inayomhusu wakili Gicheru inaibua maswali kuhusu kesi za ICC ambazo zilichangia pakubwa katika kuchaguliwa kwa Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake mwaka wa 2013.

Aidha, wachanganuzi wengi wa masuala ya kisiasa nchini Kenya wamekuwa wakijikuna vichwa kuhusiana na hatua hii na matamshi ya Fatou Bensouda na iwapo haya yatakuwa na athari katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 nchini Kenya.

Kujisalimisha kwa wakili Gicheru kwa mahakama ya ICC kulitokea miezi baada ya bwana Ruto kuonya kwamba kulikuwa na njama ya kufufua kesi dhidi yake.

Katika mahojiano yake na kituo kimoja cha televisheni nchini Kenya mnamo Januari 23 mwaka huu, Bwana Rutoa alidai, “Nilikuwa na mazungumzo na mkuu wa kitengo cha ujasusi nchini Kenya mwaka uliopita na tunavyozungumza sasa, baadhi ya watu wamewatuma watu nchini Kenya kufufua kesi za ICC lakini nataka kuwahakikishia kwamba hawatafaulu, kwa hakika, itawashangaza.”

Majuma kadhaa yaliyopita mwandani wa karibu wa Bwana Ruto, alirudia madai haya akidaia kwamba serikali ilikuwa na njama dhidi ya Bwana Ruto kwa kufanya uchunguzi ambao unaelekea kumlenga bwana Ruto.

“Waliwatuma maafisa wanne kutoka Nairobi kuchukua faili zote kuhusiana na machafuko ya mwaka wa 2007-2008. Katika machafuko hayo, watu walikufa pia eneo la Naivasha na kulikuwepo pia na machafuko maeneo ya Mombasa, Nairobi na Kisumu. Mbona wanashughulikia faili kutoka Eldoret tu?” alihoji huku maoni haya yakikubaliana na mwandani mwingine wa karibu wa bwana Ruto, mbunge wa Kapsaret, Oscar Sudi.

Hata hivyo, mkuu wa kitengo cha upelelezi nchini Kenya (DCI) George Kinoti ameshaeleza kwamba hana nia ya kufufua kesi za ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Kwenye mahakama ya ICC ingawa wakili Gicheru alijisalimisha na kuwekwa kizuizini, sasa anaitaka mahakama ya hiyo imwachilie ingawa anakabiliwa na mashtaka sita ya kuhitilafiana na kesi zilizowahusu Rais Kenyatta na Bwana Ruto kwa kuwahonga mashahidi waliohusishwa na kesi hizo.

Itakumbukwa kwamba kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya ICC wakati huo alieleza kwamba ingawa mashtaka dhidi ya Bwana Ruto yalikuwa yameondolewa, mwanya bado ulikuwepo kwa Bwana Ruto kushtakiwa siku za usoni iwapo ushahidi zaidi na mpya ungepatikana.

Wakati wakili Gicheru alipojisalimisha kwenye mahalama ya ICC maajuzi, mahakama hiyo haikueleza iwapo kuna ushahidi mpya kwani katika ripoti yake ya mwaka iliyotoa kwa Umoja wa Mataifa, mahakama hiyo ilieleza kwamba uchgunguzi ulikuwa bado ukiendelea hata ingawa kesi hizo zilikuwa zimesitishwa.

“Afisi ya mkuu wa mashataka inaendelea kupokea ushahidi kuhusu kutendeka kwa makosa ya jinai dhidi ya binadamu wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi wa Kenya wa mwaka wa 2007-2008,” ripoti hiyo ilieleza kuhusiana na shughuli za mahakama ya ICC kwenye mwaka wa 2017/2018 kuhusiana na hali nchini Kenya.

Wakili Gicheru aliambia mahakama ya ICC nchini Hague alipofika mahakamani kwa mara ya kwanza kwamba atapinga mashtaka dhidi yake, kesi yake huenda ikawa na msukumo kuhusiana na iwapo kesi dhidi ya Naibu Rais William Ruto na Joshua Sang itafufuliwa tena. Ikumbukwe kwamba, tofauti na ilivyokuwa hapo mwaka wa 2010 wakati serikali ya Kenya ilitafuta uungwaji mkono nje ya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, Kenya sasa ni mwanachama asiye wa kudumu katika baraza hilo lenye umhimu mkubwa.

Mpango wa Maridhiano wa BBI

Hali ya kisiasa na mambo mengi yamebadilika tangu kusitishwa kwa kesi hizo dhidi ya Bwana Ruto na Sang ingawa, kimsingi, wanaohusika na hali ya kisiasa iliyoko nchini Kenya kwa sasa inaelekea kukaribiana na ilivyokuwa wakati huo. Kama ilivyokuwa katika mazingira ambapo Rais Kenyatta na naibu wake walishtakiwa mwaka wa 2010, wakati kura ya maamuzi kuhusu katiba mpya ilipofanyika, wakati huu tena, Kenya inajipata katika hali ambapo huenda kura ya maamuzi ikafanywa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.

Juhudi za sasa ambazo zinafanywa chini ya mwavuli wa Mpango wa Maridhiano(BBI), unaoongozwa na Rais Kenyatta na kiongozi wa upinzani nhini Kenya, Raila Odinga, ambaye amekuwa akishirikiana na Rais Kenyatta tangu mwaka wa 2018 na kugeuza sura iliyotarajiwa kuhusiana na siasa za Kenya na mrithi wa Rais Kenyatta.

Kuhusuiana na mpango huu wa maridhiano na ripoti yake ambayo kwa sasa imetayarishiwa saini zaidi ya milioni 5 kukusanywa tayari ili kujitayarisha kwa mura ya maamuzi kuhusu katiba mwaka ujao, naibu Rais William Ruto amejikuta katika hali ngumu ya kisiasa kuhusiana na mchakato huo. Ripoti hiyo na kuwezekana kuwepo kwa kura ya maamuzi Bwana Ruto kwenye njia panda maana kuna masuala ambayo hadi sasa hajakubaliana nayo kama ambavyo hakukubaliana na kuwepo na jopo la BBI tangu mwanzo.

Kimsingi, huku shughuli za ripoti ya jopo la BBI na mchakato wa kufanyia marekebisho katiba ya Kenya zikiendelea na Bwana Ruto akijikuta kwenye njia panda kuhusiana na ripoti hiyo, uwezekano wa kuanzishwa kwa kesi inayomhusu na Bwana Sang kwenye mahakama ya ICC kutaleta changamoto nyingine kubwa kwa siasa za Bwana Ruto. Pamoja na hayo, ikumbukwe kuwa matokeo ya matukio haya mawili yana umuhimu wake kwa uchaguzi wa mwaka wa 2022.

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya sauti,

Je ripoti ya BBI ndio suluhisho la amani na umoja wa kudumu Kenya

Hali anamojikuta Bw Ruto kwa sasa inatokana na hali na mjadala kuhusu marekebisho ya katiba na kile kinachoonekana kama hali iliyotokea mwaka wa 2010 wakati kulipokuwepo na kura ya maamuzi kuhusu katiba ambapo kulikuwepo na kundi na “ndio” na lingine la “hapana”. Zaidi ni kwamba uchaguzi wa mwaka wa 2022 huenda ukapata kasi kutoka na kura ya maamuzi kuhusu katiba itakayofanyika mwaka ujao. Hali hii inaonekana kama mpangilio kabambe iliopangwa ukapangika na kumweka pabaya bwana Ruto.

Sababu mojawapo inayowafanya wandani wa Bwana Ruto kuyaona matukio ya hivi karibuni kuwa mkakati wa kisiasa ni kwamba kujisalimisha kwa wakili Gicheru kwa mahakama ya ICC na juhudi zinazoonekana kama zile zenye nia ya kufufua kesi dhidi ya Bwana Ruto kwenye mahakama hiyo zote zinatokea wakati ambapo Bwana Odinga na Bwana Ruto wanaonekana kupanga mikakati ya kujipanga kwenye maeneo mbali mbali nchini Kenya kujitayarisha kwa uchaguzi wa mwaka wa 2022 na kura ya maamuzi kupitia kwa BBI ili kurekebisha katiba ya Kenya.

Kwa sasa, inavyoonekana, kuna masuala mengi ambayo huenda yakabadilisha mkondo siasa za Kenya lakini ukweli ni kwamba, kwenye siasa za Kenya, mkoko ndio mwanzo unaalika maua.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *