img

Japan inapanga kuinua kiwango chake cha uzazi wa watoto

December 8, 2020

Japan inapanga kuinua kiwango chake cha uzazi wa watoto kinachopunua kwa ufadhili intelijensia bandia ya mfumo wa kufananisha ili kuwasaidia wakazi kuwapata wapenzi.

Kuanzia mwaka ujao serikali ya nchi hiyo itazisaidia serikali za majimbo ambazo tayari zimeanza kuendesha mfumo huo au kuanzisha miradi ambayo inatumia Intelijensia bandia kuwakutanisha watu.

Mwaka jana idadi ya watoto wachanga waliozaliwa nchini Japan ilishuka chini ya 865,000 – ikiwa ni rekodi ya chini kuwahi kushuhudiwa.

Nchi hiyo ambayo ina idadi kubwa ya watu wanaozeeka kwa haraka kwa muda mrefu imekuwa ikitafuta njia za kupunguza viwango vya chini zaidi vya uzazi duniani vinavyoshuhudiwa katika taifa hilo.

Kuongeza matumizi ya teknolojia ya Intelijensia bandia (IT) ni moja ya juhudi zake za hivi karibuni kujaribu kukabiliana na tatizo hilo.

Mwaka ujao serikali inapanga kuzitendea mamlaka nchini humo yen bilioni 2 (dola milioni 19 ) ili kuinua kiwango cha uzazi , limeripoti shirika la habari la AFP

Tayari mamlaka kadhaa zinaendesha huduma za kuwakutanisha watu na baadhi zimeanzisha mifumo ya Intelijensia bandia kwa matumaini kwamba itafanya tathmini ya kisiri zaidi ya kuweka mfumo ambapo watu watakuwa wakiwasilisha maelezo yao.

Michache kati ya mifumo iliyopo ina uwezo mdogo wa kuangalia vigezo kama vile mapato na umri, ikitoa matokeo tu kama maelezo ya watu wawili yataonana yote.

Vyombo vya habari nchini humo vinasema ufadhili huo unalenga kuziwezesha mamlaka kuimarisha mifumo ya gharama zaidi ambayo itaangalia pia mambo kama vile vitu ambavyo mtu anapenda kufanya na maadili yake ili kuweza kumpata mpenzi anayefanana naye.

“Tunapanga hususan kutoa ruzuku kwa huduma za serikali za mitaa au miradi inayoanza kutoa huduma za Intelijensia bandia ya kuwakutanisha watu na wapenzi wao ,” afisa wa wizara aliliambia Shirika la habari la AFP. “Tunamatumaini kuwa usaidizi huu utasaidia kupunguza kushuka kwa viwango vya uzazi wa watoto katika taifa hili ,”

Idadi ya watu nchini Japan inakadiriwa kushuka kutoka watu milioni 128 million katika mwaka 2017 hadi chini ya watu milioni 53 ifikapo mwishoni mwa karne hii.

Watungasera wanahangaika kuhakikisha kuwa watu wenye nguvu za kufanya kazi wanaweza kuhimili garama zinazoongezeka za maisha.

Sachiko Horiguchi, mtaalamu wa masuala ya kijamii na utamaduni na mtaalamu wa tiba ya watu katika Chuo Kikuu Temple nchini Japan, anafikiri kuna njia bora kwa serikali za kuongeza kiwango cha uzazi wa waroro kuliko kugarimia Intelijensia bandia ya kuwafananisha watu-kama bile kuwasaidia vijana kupata mshahara mdogo.

Amezungumzia ripoti ya hivi karibuni inayoelezea uhusiano wa viwango vya chini vya mishahara na ukosefu wa utashi wa mapenzi miongoni mwa vijana watu wazima nchini Japan.

“Kama hawataki kuchumbia, kuwatafutia watu wenye vigezo vinavyofana na na vyao huenda kusiwe na ufanisi wowote,” Dkt Horiguchi aliiambia BBC. “Kama tunategemea teknolojia, roboti nafuu za intelijensia bandia kufanya kazikwa kazi za nyumbani au kazi za watoto inaweza kuwa na ufanisi.”

Wachambuzi kwa muda mrefu wamekuwa wakielezea kuhusu ukosefu wa usaidizi kwa akinamama wafanyakazi nchini Japan, ambapo kuna matarajio makubwa kuwa mwanamke anapaswa kufanya kazi zote za nyumbani na kuwakuza watoto wakati huo huo akifanya kazi nyingine bila usaidizi.

Serikali imesema kuwa inataka kuwahamasisha wanawake kufanya kazi za kuajiriwa kwa muda kamili wa kazi katika miaka ya hivi karibuni lakini pengo la jinsia limeendelea kupanuka katika soko la ajira.

Japan iliwekwa namba 121 katika nchi 153 katika ripoti ya mwaka 2019 ya usawa wa jinsia na Jukwa la kiuchumi la dunia- World Economic Forum, ikishuka nafasi 11 kutoka mwaka uliotangulia.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *