img

Fahamu Mikoa inayoongoza kwa matukio ya Ukatili

December 8, 2020

 

Ukatili wa kijinsia umetajwa kuwa chanzo cha Serikali kupoteza fedha nyingi katika kuhudumia wahanga pamoja na kuendesha kesi hizo nchini, hali inayo kwamisha baadhi ya huduma kutokana na pesa hizo kupotea huko.

Hayo yameelezwa na Spika wa Bunge Mstaafu, Anna Makinda, wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia pamoja na maadhimisho ya miaka 25 ya Beijing leo Desemba 8, 2020 Jijini Dar es Salaam.

Akitoa takwimu za matukio ya ukatili nchini amesema kuwa, kwaa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu mwaka 2015-2016 unaonesha kuwa asilimia 40 ya wanawake wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi 49 wameshafanyiwa vitendo vya ukatili wa kupigwa au kingono katika maisha yao.

“Kama tunavyopambana katika mambo mengine, tuandae pia kizazi chenye kuleta mapinduzi ya kijinsia ili Ukatili wa kijinsia uwe historia Tanzania na Duniani, Takwimu hizo pia zilionesha mikoa inayoongoza kwa matukio ya ukatili wa kijinsia ni, Kagera, Mara, Mwanza na Kigoma”, amesema Makinda.

Akizungumzia miaka 25 ya Beijing pamoja na hali ya matukio ya ukatili Tanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi amesema kuwa Watanzania wanatakiwa kuongeza nguvu katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *