img

Diwani kupitia Chadema aapishwa adai kutopokea barua ya kumzuia

December 8, 2020

NA Amiri Kilagalila,Njombe

Diwani pekee kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kutoka kata ya Uhenga kati ya madiwani 28  wa halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe ameapishwa pamoja na madiwani wengine wa Chama cha Mapinduzi licha ya Chama chake kuendelea na msimamo wa kuto tambua madiwani na mbunge walioshinda katika nafasi hizo kwa madai ya uchaguzi uliopita kuto kuwa wa huru na haki.

Katika kikao Cha kwanza Cha Baraza maalamu la madiwani Halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe kilichofanya kazi ya Kuwaapisha madiwani hao,Kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri na Makamu wake pamoja na Kamati mbalimbali kimewachagua pia Agnetha Mpangile Diwani wa kata ya Ulembwe kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri na Makamu wake Onesmo Lyandala ambaye Ni Diwani wa kata ya Imalinyi Huku Hakimu mkazi mahakama ya mwanzo Makambako na Mdandu Almachius Kasaizi Wakati akiwaapisha amewataka kwenda kukitumikia kiapo.

“Majukumu mnayoenda kuyafanya ni kuyatekekeleza kwa mujibu wa sheria,uadilifu na uaminifu” alisema Almachius Kasaizi hakimu mkazi mahakama ya mwanzo Makambako na Mdandu wakati akiwaapisha madiwani

Chadema kupitia Kamati kuu kilitangaza kutotambua madiwani na mbunge walioshinda nafasi zao kwenye uchaguzi mkuu wa October 28 mwaka huu huku Diwani wa kata ya Uhenga bwana Alfan Kawambwa amekula kiapo kwa madai  ya kuto kuwa na  barua ya kumzuia kwenda kuapishwa.

“Kutokana na matamkoa mbali mbali ya Chama changu,sina barua rasmi ya kunizuia kuja kuapa,kwa hiyo nimekuja kuapa nikiwa na baraka zote kama diwani wa kata ya Uhenga,Nimeingia ukumbini mpaka ninaapa sikuwa na barua yeyote inanizuia nisile kiapo cha uaminifu kama diwani wa kata ya Uhenga”Alisema  Alfan Kawambwa

Baadhi ya madiwani kupitia Chama Cha mapinduzi CCM akiwemo Thobias Mkane Annaupendo Gombela na Syrevester Kigora  Wamesema hata Kama Halmashauri hiyo imempata Diwani Mmoja toka Chadema lakini wanaamini kuwa Hali itakuwa shwari kwa kuwa lengo Lao Wote Ni kuwaletea maendeleo Wananchi.

“Kuwepo mwenzetu wa upinzani hili halitaathiri hata sehemu moja utendaji wa kazi za halmashauri kwasababu tutafanya kazi kwa mujibu wa miongozo ya serikali na tunachoaidi sisi ni maendeleo kwa wananchi”alisema Thobias Mkane

Siku chache zilizopita mwandishi wetu alizungumza na mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Rose Mayemba, juu ya taarifa za madiwani wake kwenda kuapishwa ambapo alisisitiza msimamo wa Chama hicho kwa madiwani wao wa kata 4 waliochaguliwa mkoani humo kuendelea kuzingatia utaratibu huku akieleza kuchukuliwa hatua watakapokiuka utaratibu.

“Kama ambavyo katibu mkuu wa Chama chetu alivyozungumza juu ya wote walioshinda kwenye nafasi zao Chama hakijabadirika bado kwamba hawatambuliwi wabunge na hawatambuliwi madiwani” Alisema Rose Mayemba

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *