img

Burundi yawapokea wawakilishi wa EU

December 8, 2020

Burundi na Muungano wa Ulaya (EU) zimekubali kurejelea tena mashauriano kwa lengo la kurejesha uhusiano wa kidiplomasia baada ya kusitishwa miaka mitano iliyopita, ofisi ya rais imetangaza.

Rais Evariste Ndayishimiye siku ya Jumatatu alikutana na wawakilishi wa EU nchini Burundi pamoja na mabalozi kutoka nchi za Ulaya.

Pande hizo mbili “zilikubaliana kusahau yaliyopita na kuangazia siku zijazo kwa kujenga upya uhusiano wao”, kwa mujibu wa afisi ya rais.

Burundi ilikuwa imeilaumu EU kwa “kudhamini misukosuko” nchini humo kufuatia jaribio la mapinduzi lililotibuka mwezi Mei mwaka 2015. EU ilikatiza msaada wa bajeti kwa serikali kutoka na kile ilitaja kuwa ukiukwaji wa haki za binadamu.

Rais Pierre Nkurunziza alikuwa madarakani wakati huo. Alifariki mapema mwaka huo na nafasi yake kuchukuliwa na rais Ndayishimiye.

Balozi wa EU mjini Bujumbura Claude Bochu ameweka picha ya mkutano huo katika Tweeter yake, na kusema kuwa ulifanyika katika “mazingira tulivu na ulikuwa wa kufana”.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *