img

ATCL mbioni kuanza safari za ndege Geita

December 8, 2020

 

Mamlaka  ya Anga Tanzania (TCAA)  na Shirika la Ndege nchini (ATCL) wamekutana kujadili kuanza kwa safari za ndege katika uwanja wa ndege wa Geita.

Mkaguzi wa viwanja vya ndege kutoka TCAA,  Bernard Kavishe akizungumza leo Jumanne Desemba 8, 2020 wakati wa mkutano wa wakuu wa taasisi kuhusu uanzishwaji wa huduma za usafiri wa anga mkoani Geita,  amesema lengo la mkutano huo ni kwa ajili ya kuangalia utayari wa uwanja huo ili uweze kuanza safari.

Mtendaji mkuu wa ATCL,  Ladislaus Matindi amesema lengo la kukutana ni kujadili utayari wa uwanja wa ndege huo ili kuona wao wafanye nini katika kuhakikisha wateja wao wanapata usafiri karibu na haraka.

Amesema  utaziwezesha ndege za ATCL kuruka na kutua Chato na kuwataka wakazi wa mkoa wa Geita kuwa tayari kwakuwa shirika hilo litaanza safari zake wakati wowote kuanzia sasa.

Awali, akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo meneja wa wakala wa barabara mkoani Geita,  Haroun Senkuku amesema uwanja huo wenye urefu wa kilomita sita na upana wa kilomita moja umegharimu zaidi ya Sh58 bilioni ambazo ni fedha zinazotokana na mapato ya ndani.

Amesema kazi zilizo fanyika ni ujenzi wa njia za kutua na kuruka ndege, ujenzi wa eneo la maegesho ya ndege ,ujenzi wa eneo la usalama, ujenzi wa kuweka alama eneo la kuruka na kutua ndege pamoja na ujenzi wa jengo la wageni maalum.

Akifungua mkutano huo mkuu wa mkoa wa Geita, Robert Gabriel amesema uwanja wa Geita ni wa kipekee kwa sababu ni miongoni mwa viwanja vya kwanza kujengwa kwa mapato ya ndani na kwa kutumia wataalam wa serikali pamoja na mkandarasi mzawa.

Amesema uwanja huo utakua chachu ya maendeleo ya Mkoa wa Geita pamoja na mikoa jirani lakini pia utakuwa kitovu cha kuunganisha Tanzania na nchi jirani za Uganda, Rwanda na Burundi.

Gabriel amesema mkutano huo wa wataalam utahakikisha utayari wa kiwanja cha mkoa wa Geita kuanza kutoa huduma za kibiashara za usafiri wa anga.

Amebainisha kuwa huduma ya usafiri wa anga itakua fursa adimu kwa wafanyabiashara, wakulima na wananchi kusafiri na kusafirisha mazao na bidhaa zao na kuzifikisha kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi kwa haraka.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *