img

Waziri Mkuu afanya ziara Hospitali ya Uhuru, aagiza huduma zianze kutolewa Desemba 20

December 7, 2020

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa amekagua umaliziaji wa ujenzi wa Hospitali ya Uhuru unaoendelea katika wilaya ya Chamwino, Dodoma na kuagiza huduma zianze kutolewa ifikapo Desemba 20 mwaka huu.

Amekagua hospitali hiyo na kuagiza kwamba vifaa vyote zikiwemo samani na vifaa tiba vinavyotakiwa kuwepo kwenye hospitali hiyo vipelekwe na vifungwe ili huduma zianze kutolewa.

Desemba 3 mwaka huu Rais Dkt. Magufuli aliahirisha maadhimisho ya sherehe za miaka 59 Uhuru zilizotarajiwa kufanyika Desemba 9, 2020 na kuelekeza kiasi cha shilingi milioni 835,498,700 zilizotengwa kwa ajili ya sherehe za hizo zitumike kununulia vifaa mbalimbali kwa ajili ya Hospitali ya Uhuru.

Licha ya ununuzi wa vifaa hivyo, pia Mhe Rais Dkt. Magufuli aliagiza fedha hizo zitumike kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa kuzunguka eneo la hospitali hiyo pamoja na ujenzi wa barabara ya kuingilia hospitalini hapo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge aliishukuru Serikali kwa uboreshaji wa huduma za afya mkoani Dodoma ukiwemo ujenzi wa hospitali hiyo ya Uhuru, ambapo ameiomba iwaongezee wataalamu wa afya.

Hadi kufikia sasa ujenzi wa hospitali hiyo ya Uhuru umegharimu shilingi bilioni 4.2. Januari 2019 wakati akipokea gawio la hisa za kampuni ya Simu ya Airtel Rais Dkt. Magufuli aliagiza kiasi cha shilingi 2,415,151,650.00 zilizotolewa na kampuni hiyo zitumike katika ujenzi wa hospitali hiyo.

Novemba 20, 2018, Rais Dkt. Magufuli aliagiza kiasi cha Tsh. milioni 995,182,000.00 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 57 ya Uhuru zitumike kujenga Hospitali ya Uhuru, ambayo kwa sasa ujenzi wake upo katika hatua za umaliziaji

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *