img

Watu 140 walazwa baada ya kuugua ugonjwa wa ajabu India

December 7, 2020

 

Maofisa nchini India wanachunguza ugonjwa ambao haujafahamika uliosababisha zaidi ya watu 140 kulazwa mwishoni mwa wiki hii.

Wagonjwa hao kutoka mji wa Eluru huko Andhra Pradesh, wamekuwa na dalili za kichefuchefu na kukosa nguvu, daktari ameeleza.

Hospitali ya serikali ya Eluru imetenga vitanda kadhaa kwa ajili ya wagonjwa wa ugonjwa huo usiojulikana kama vitahitajika.

Ugonjwa huo unakuja wakati India ikiwa inakabiliwa na mlipuko wa janga la corona.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa wagonjwa hao walifanyiwa vipimo vya corona na wote wakawa hawana.

Maafisa wa afya wa hospitali ya Eluru wameiambia ‘The Indian Express’: “Watu wa India wanaugua, haswa watoto , ghafla tu wanaanza kutapita baada ya kulalamika kuwa macho yao yanawasha.

Wengine wanazimia au kukosa nguvu kabisa.

Wengi wao waliopelekwa hospitali wanaonekana kupona kwa haraka na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Waziri wa afya wa Andhra Pradesh Alla Kali Krishna Srinivas alisema sampuli za damu zao hazikuona ushaidi wowote wa maambukizi yatokanayo na virusi.

“Tunachunguza maji na hewa katika eneo ambalo watu wanaugua ugonjwa huo,” alisema. “Ugonjwa huu wa ajabu utadhibitika tu mara tu matokeo ya maabara yatakapotoka.”

Hata hivyo wanasiasa wa upinzani kutoka chama Telugu Desam ,wametaka ufafanuzi wa sababu ya kuibuka kwa ugonjwa huo wa ajabu.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *