img

Wanne mkoani Manyara Jeshi washikiliwa kwa kukutwa na Jino la Tembo

December 7, 2020

Na John Walter-Manyara

Jeshi la polisi mkoani Manyara, linawashikilia watu wanne wakazi wa  wilayani Mbulu mkoani hapo, baada ya kukutwa na jino moja la Tembo wakijiandaa kuliuza.

Taarifa kutoka jeshi la Polisi imeeleza kuwa mnamo Desemba 6,2020 katika kijiji cha Sanu kata ya Sanu tarafa ya Endagikoti Zone 17 wilayani Mbulu, askari wakiwa kazini walipata taarifa za kiintelijinsia kuhusu watu waliokuwa kwenye harakati za kutaka kuliuza Jino hilo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Paul Kasabago amewataja watuhumiwa hao ni Gobre Haniiti (18) mkazi wa Haisary, Lagoo Selestini (34) mkazi wa Mwanga mkoani Singida, Safari Hamsi (35) mkazi wa Haisary na Paulo Gidioni (30) mkazi wa Mwanga mkoa wa Singida.

Kamanda Kasabago amesema watuhumiwa wote hao walikuwa na Kipande cha Jino la Tembo lenye uzito wa Kilogram 1.420 ambayo thamani yake bado haijajulikana.

Amesema watuhumiwa wote wamekamatwa na Upelelezi utaapokamilika watafikishwa mahakamani.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *