img

Wananchi wa kata za Nakahako,Mikumbi na Chilangala walalmikia kutokamilika kwa wakati kwa mradi wa maji

December 7, 2020

Na Faruku Ngonyani,Mtwara

Wananchi wa kata ya Nakahako, Mikumbi na Chilangala Zilizopo Halmashauri ya Wilaya Newala Mkoani Mtwara wamelalamikia kutokamilika kwa wakati  mradi wa maji lukohe na mnima miyuyu ulioanza kutekelenzwa  2018 na mamlaka ya usambazaji maji na usafi wa mazingira RUWASA ambapo mradi huo ulitakiwa kukamilika ndani ya miezi tisa  tangu kuanza kwake

Wakizungumza katika kongamano la ushawishi na utetezi katika kuziangazia changamoto za miradi ya Maji Lukohe na mnima Miyuyu lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la NEHIA kupitia Mradi wa Medi kwa Maendeleo vijijini wamesema hawatarajii kuona Maji yakitoka katika maeneo yao kutokana na uwepo wa changamoto hiyo kwa muda mrefu

Kwaupande wao Madiwani kata hizo wametoa Rai ya kuchukua hatua kwa wakandarasi na  kuchunguzwa  waliotekeleza mradi huo kutokana na  kukamilika na kushindwa kutoa maji

Aidha wamesema Mradi huo wa Lukohe  na Mnima Miyuyu kwa kata ya Mikumbi umegharimu kiasi cha shl bil 5.9 kwa kata ya Chilangala bil5.9 na Nahahako  bil 2.29 ambapo wakandarasi wamehitimisha lakini hautoi maji kutokana na changamoto zinanazojitokeza

Aidha madiwani hao wameliomba shirika la NEHIA kuendelea kufuatilia mradi huo ili waweze kuwasaidia.

Akieleza kuhusiana na mradi huo kaimu Meneja wa mamlaka ya usambazaji Maji na usafi wa Mazingira mjini na vijijini RUWASA  ENG Juma Hassani Musaa ameagidi kuwa na kusema kuwa ifikapo Disemba 31 mwaka huu utakuwa umekamilika na wananchi watapata maji

Kwa upande wake mwenzeshaji kutoka shirika NEHIA Peter Kibehi ameahidi kuendelea kufuatilia miradi hiyo maji.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *