img

Virusi vya corona: Wakili wa Trump Rudy Giuliani alazwa hospitali kwa Covid-19

December 7, 2020

Dakika 3 zilizopita

Rudy Giuliani

Maelezo ya picha,

Rudy Giuliani amesafiri maeneo tofauti kuwasilisha kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi wa mwezi uliyopita

Wakili wa kibinafsi wa rais Donald Trump, Rudy Giuliani, amepatikana na virusi vya corona na kwa sasa ana pokea matibabu hospitalini.

Rais aliandika katika Twitter yake: “Nakutakia afueni ya haraka Rudy, tuendelee mbele!”

Bwana Giuliani, ambaye amekuwa akiongoza harakati za kampneia ya Trump kupinga kisheria matokeo ya uchaguzi, ni mwandani wa karibu wa wa rais kuambukizwa virusi virusi hivyo.

Rais na kundi lake wameakosolewa kwa kutozingatia mwongozo wa kijikinga na dhidi ya virusi vya corona. Bwana Trump alipata virusi hivyo hatari mwezi Oktoba.

Bwana Giuliani, 76, alilazwa katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Medstar Georgetown mjini Washington DC siku ya Jumapili, kwa mujibu wa ripotiza vyombo vya habari nchini Marekani.

Katika ujumbe wa twitter, meya huyo wa zamani wa New York aliwashukuru watu waliomtumia ujumbe wa kumtakia uponaji wa haraka na kusema kuwa “anaendelea kupata nafuu”.

white space

Mwanawe wa kiume, Andrew Giuliani, ambaye anafanya kazi White House alipatikana na virusi vya corona mwezi uliyopita, ameandika katika twitter yake akisema baba yake “anapumzika baada ya kutunzwa vizuri na anajihisi vyema”.

white space

Haijabainika ikiwa Bwana Giuliani anakabiliwa na dalili za ugonjwa huo au ni linialipata maambiukizi ya virusi.

Karibu watu milioni 14.6 nchini Marekani wamethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Covid-19, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, na watu 281,234 wamefariki – idadi ambayo ni ya juu zaidi kushuhudiwa katika nchi nyingine yoyote duniani.

Siku ya Jumapili, Dkt Deborah Birx, mshirikishi wa jopo kazi la White House kuhusu virusi vya corona, alikosoa utawala wa Trump kwa kukiuka muongozo wa kuzuia maambukizi na kuendesha “dhana potofu” kuhusu janga la corona.

“Nasikia watu katika jamii wakipiga domo kuhusu mazingira yanayosababisha maambukizi, wakisema barakoa hazifanyi kazi, wengine wakisema tunahitaji kuangazia juhudi zetu katika kinga imara mmwilini,” Dkt Birx aliambiaNBC.

“Hili ni tukio baya zaidi ambalo nchi hii itakabiliwa nayo,” alisema.

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya video,

Mambo matano muhimu kuhusu virusi vya corona

Tangu uchaguzi wa Novemba 3, wakili huyo amesafiri maeneo tofauti katika juhudi za kubatilisha matokeo ya uchaguzi bila mafanikio. Wakati mwingi alionekana bila barakoa na kupuuza kutokaribiana na watu.

Alhamisi iliyopita alisafiri hadi Georgia ambako bila ya kuwa na ushahidi wowote alidai kulikuwa na wizi wa kura mbele ya kamati ya Bunge la Seneti linalochunguza kuhusu uhalali wa uchaguzi.

Watu kadhaa wa karibu na Bwana Trump wamedaiwa kuambukizwa virusi vya corona tangu mwezi Octoba.

Boris Epshteyn, mshauri mwingine wa Trump, alipatikana na virusi muda mfupi baada ya kufanya mkutana na wanahabari akiwa Rudy Giuliani Novemba 25.

Wengine ni pamoja na mkuu wa watumishi wa rais Mark Meadows na waziri wa habari Kayleigh McEnany, pamoja na mke wa rais Melania na wanawao wa kiume Donald Jnr na Baron.

Bwana Trump hajakubali kushindwa uchaguzi, akisisitiza bila ya kuwa na ushahidi kwamba ushaguzi ulikumbwa na udanganyifu au kura kuibwa. Mwanasheria Mkuu William Barr, wiki iliyopita alisema ofisi yake haijapokea ushahidi wowote unaoashiria wizi wa kura ambao huenda ukabadilisha matokeo ya uchaguzi.

Bwana Biden ataapishwa rasmi kuwa rais Januari 20 mwaka 2021.

Coronavirus

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *