img

Umoja wa Ulaya wajadili uwezekano wa kuiwekea Uturuki vikwazo

December 7, 2020

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wamejadili uwezekano wa kuiwekea vikwazo Uturuki kuhusiana na mzozo wa gesi katika eneo la mashariki mwa Mediterenia, kabla ya viongozi wa Umoja huo kufanya uamuzi juu ya suala hilo katika mkutano wa kilele utakaofanyika Disemba 10-11.

Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan amesema nchi yake haitatishika lakini amerudia wito wake wa kufanyika mazungumzo juu ya suala hilo la mzozo wa raslimali.

Mzozo uliibuka mnano mwezi Agosti baada ya Uturuki, ambayo ni mwanachama wa jumuiya ya kujihami ya NATO, kutuma meli ili kufanya utafiti wa raslimali katika eneo inalolizozania na Ugiriki.

Ujerumani ambayo inashikilia Urais wa kupokezana wa Umoja wa Ulaya kwa muda wa miezi sita, ndiyo yenye uamuzi wa mwisho wa iwapo vikwazo hivyo dhidi ya Uturuki vitawekwa au la.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *