img

Ujerumani yasema chanjo ya Covid-19 kuanza kutolewa mapema Januari

December 7, 2020

Kiongozi wa wafanyikazi katika ofisi ya Kansela wa Ujerumani amesema anatarajia chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 kuanza siku za mwanzo za mwaka mpya.Helge Braun, ambaye pia ni daktari kitaaluma ameliambia gazeti la The Bild kuwa yuko tayari kusaidia katika utoaji wa chanjo hiyo.

Mamlaka za Umoja wa Ulaya zinatarajiwa kufanya uamuzi juu ya kuidhinisha matumizi ya chanjo mnamo Disemba 29.Tayari Ujerumani imeanza kuweka vituo maalum vya kutoa chanjo hiyo.

Leo Jumatatu, Taasisi ya Ujerumani ya kudhibiti magonjwa ya Robert Koch imesema watu 12,332 wameambukizwa virusi vya Corona katika saa 24 zilizopita, ikiongezeka kutoka watu 11,168 wiki iliyopita, na vifo 147.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *