img

Uingereza na Umoja wa Ulaya kujaribu kete ya mwisho ya makubaliano ya Brexit

December 7, 2020

Uingereza na Umoja wa Ulaya wiki hii wanatarajiwa kuingia katika jaribio la mwisho la makubaliano ya kibiashara ya baada ya Brexit, zikiwa zimesalia siku chache kwa wajumbe wa makubaliano hayo kujadiliana ili kuepusha Brexit ya bila makubaliano. 

Waziri mkuu wa Ireland, ambaye taifa lake huenda likakabiliwa na hali ngumu zaidi ya uchumi kuliko mengine 26 wanachama wa umoja huo, iwapo kutakuwepo na Brexit ya bila kukubaliana, ameonya kuhusiana na matumaini yaliyoko juu ya mchakato huo. 

Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson na rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen wamezungumza mwishoni mwa wiki hii ili kuwarejesha wawakilishi wao kwenye majadiliano hayo baada ya kukwama kufuatia kutokukubaliana kwenye masuala matatu ya msingi. 

Wakuu hao wanatarajiwa kuzungumza tena baadaye leo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *