img

Uchaguzi Uganda 2021:Ghasia bado zinaendelea Uganda

December 7, 2020

Bobi Wine ameiambia BBC kuwa yeye na wafuasi wake walishambuliwa tena na polisi alipoenda kufanya kampeni huko Luhuka ,eneo alilokamatwa mwezi uliopita.

Bobi Wine amesema kitendo hicho ni cha kinyama “watu kadhaa wamejeruhiwa akiwa pamoja na rafiki yangu wa karibu alipigwa na mtungi wa gesi ya kutoa machozi na kuumia sana, ila ni wengi wameathirika na wengine kuuawa”.

Ameongeza kusema kuwa hatakubali kuona kuwa rais Museveni anaingiia kati mchakato wa uchaguzi.

Lakini amesisitiza kuwa atadai haki zao bila kufanya vurugu, “Hatuamini vurugu , tunadharau vurugu hivyo hatuna nia ya kuchukua silaha na kufanya vurugu”.

Gazeti la Daily Monitor nchini Uganda limenukuu Tweeter ya Robert Kyagulanyi aliyosema “Hii ni vita , sio kampeni za uchaguzi.”

Raia wa Uganda wanatarajia kupiga kura Januari 14, 2021.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *