img

Uchaguzi Ghana: Mambo sita unayopaswa kufahamu

December 7, 2020

Dakika 7 zilizopita

Ukosefu wa ajira kwa vijana, wasiwasi wa usalama na athari za janga la Covid-19 juu ya uchumi ni miongoni mwa masuala yatakayozingatiwa na Waghana wakati wa kupiga kura.

Raia wa wanaenda kupiga kura kuchagua rais mpya na bunge katika nchi inayoonekana kama moja ya nchi zenye demokrasia zaidi Afrika Magharibi.

Wagombea kumi na mmoja wako katika kinyang’anyiro cha kumshinda Rais Nana Akufo-Addo, anayewania muhula wake wa pili.

Mpinzani wake mkuu ni mtangulizi wake na mpinzani wa 2016, John Dramani Mahama.

Ukosefu wa ajira kwa vijana, wasiwasi wa usalama na athari za janga la Covid-19 juu ya uchumi ni miongoni mwa masuala yatakayozingatiwa na Waghana wakati wa kupiga kura.

Hapa kuna mambo sita ya kujua kuhusu uchaguzi huu.

Ulimwengu umepitia mashaka mengi na mshangao mwaka huu lakini mbio za urais wa Ghana zinajulikana sana.

Mgombea wa chama tawala cha New Patriotic Party (NPP), Bw Akufo-Addo, 76, na mpinzani wake wa muda mrefu, Bw Mahama, 62, wa National Democratic Congress (NDC), wanawania tena kwa mara ya pili na ya tatu mahasimu hao wawili walipambana mnamo mwaka 2012.

Katika mchuano wa kwanza, Bwana Mahama bila kutarajia alikua mgombea wa chama chake baada ya wakati huo Rais John Evans Atta Mills kuaga dunia miezi mitano tu kabla ya mchakato wa kupiga kura

Rais wa Ghana na mgombea wa chama cha New Patriotic Party (NPP) Nana Akufo-Addo

Bwana Mahama, 62, alipinga ushindi Bw Akufo-Addo, mwenye umri wa miaka 76.

Matokeo yalipingwa kortini msingi wa madai ukiwa udanganyifu wa uchaguzi lakini baada ya miezi nane Mahakama Kuu ya Ghana iliunga mkono ushindi mdogo wa Bw Mahama.

Rais wa zamani wa Ghana John Dramani Mahama

Maelezo ya picha,

Mr Mahama admits that lapses in his campaign four years ago cost him the re-election

Hatahivyo, Bw. Akufo-Addo, alilipiza mwaka 2016.

Hii itakuwa mara ya kwanza tangu demokrasia kuanzishwa tena mnamo 1992 – baada ya miaka ya utawala wa kijeshi – kwamba uchaguzi utafanyika bila ushawishi wa rais wa zamani wa zamani Jerry Rawlings

Kiongozi huyo mwenye haiba na umaarufu, ambaye alisimamia kurudi kwa siasa za vyama vingi, alifariki akiwa na umri wa miaka 73 katika hospitalini katika mji mkuu, Accra, tarehe 12 mwezi Novemba baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Jerry Rawlings mwaka 2001

Ingawa Rawlings aliunga mkono chama tawala NPP katika uchaguzi wa mwaka 2016, waangalizi wa masuala ya kisiasa wamesema chama cha Bw. Mahama, NDC, kilichoanzishwa na Rawlings, kinapata kura za huruma.

Rawling kumuunga mkono Bwana Akufo-Addo kulisababisha hali ya kukosa imani ndani ya chama cha upinzani hali iliyogharimu kura za chama hicho.

Zaidi ya watu 80,000 wanaokiunga mkono NDC katika majimbo mbalimbali katika mkoa wa Volta, ulio ngome ya chama, hawakupiga kura katika uchaguzi wa mwaka 2016, Bw.Mahama aliiambia BBC idhaa ya Pidgin.

Kabla ya kifo cha Rawlings, NDC kilifanya jitihada ya kusawazisha mahusiano yake naye na maafisa wa chama sasa wanasema wana uhakika kuwa wataepuka kurejea kwa hali ya kutojali .

Lakini kunaweza kuwa na ugumu: Nana Konadu Agyeman-Rawlings, mjane wa rais wa zamani, ndiye mgombea urais wa Chama cha National Democratic Party (NDP).

3. Uchaguzi wa kwanza bila ‘makundi ya wafanya vurugu’

Kuna hali ya unafuu katika nchi ambayo kuchaguzi hautakumbwa na mapigano yanayosababishwa na makundi ya watu walioajiriwa na wanasiasa.

Sheria iipitishwa mwaka jana kuunga mkono kupigwa marufuku uwepo wa makundi ya vurugu na kutangaza adhabu ya kifungo si chini ya miaka kumi kwa watakaohusika.

Vyama vikuu viwili vimeshutumiwa kwa kuwakodi vijana wenye nguvu ili ”kulinda kura.”

Badala yake wamekuwa na sifa ya kutumia vitisho na vurugu dhidi ya wapinzani.

4. nchi ya Western Togoland

Hata hivyo, kivuli kilichopo hivi sasa ni makundi yanayotaka kujitenga, ambayo yamekazana kutaka uhuru wao kutoka Ghana na kuunda nchi yao-Western Togoland.

Map

Wito wa kujitawala uliibuka tena mnamo 2017 – baada ya mapumziko ya karibu miongo miwili – wakati vikundi viwili zaidi vya wapiganaji viliundwa.

Mnamo Septemba, moja ya vikundi vipya, Western Togoland Restoration Front (WTRF), kilifanya vurugu kwa mara ya kwanza katika historia ya harakati ya kujitenga.

Iliweka vizuizi barabarani, ikashambulia kituo cha polisi, ikamata silaha na kuteketeza kituo cha basi.

Serikali imepeleka wanajeshi katika Mkoa wa Volta kabla ya uchaguzi ili kuzuia jaribio lolote la kuvuruga uchaguzi.

5. ‘Orodha ya Ecowas ‘ yasafishwa

Tume ya Uchaguzi ya Ghana iliandaa daftari jipya la wapiga kura kabla ya kura ili kujaribu kuwaondoa raia wa kigeni wanaoshukiwa kuongezwa – likipatiwa jina la “daftari la Ecowas” -ikiashiria Jumuia ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ambayo Ghana ni mwanachama.

Mwezi Juni, jeshi lilipelekwa kwenye maeneo ambayo ni ngome ya wapinzani katika miji ya mpakani mkoani Volta kabla ya zoezi la kusajili wapiga kura ili kupeleka ulinzi.

Mwezi Juni, wanajeshi walipelekwa katika ngome za upinzani katika miji ya mpakani katika Mkoa wa Volta kabla ya zoezi la uandikishaji wapigakura kutoa usalama.

Jean Mensa

Maelezo ya picha,

Jean Mensa has denied claims of prejudice against people from opposition strongholds

NDC ilishutumu tume hiyo kwa kujaribu kuwanyang’anya haki watu ambao wana uraia wa nchi mbili, hasa wale wa Ghana na Togo.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jean Mensa alikanusha madai ya chuki dhidi ya watu kutoka Mkoa wa Volta.

Wapiga kura milioni mbili zaidi wanapiga kura kura katika uchaguzi wa leo ikilinganishwa na miaka minne iliyopita.

Mnamo mwaka wa 2016 tume ya uchaguzi ya Ghana ilipata sifa duniani kote kwa kusimamia vizuri mchakato wa uchaguzi.

Mamlaka wanajua sifa hii na watataka kuhakikisha wanatimiza matarajio.

6. Kampeni wakati wa janga la corona

Janga hilo lilibadilisha namna ambavyo kampeni hufanyika kampeni zilifanywa – hali ambayo imewakatisha tamaa wanasiasa na Umma.

Badala ya mikutano ya hadhara, ya kupendeza na yenye kusisimua, vyama vya siasa vimetumia mitandao ya kijamii kama Twitter na video kuwasilisha ujumbe.

Supporters of incumbent president and presidential candidate the leader of the New Patriotic Party (NPP) Nana Akufo-Addo attend an election rally in Kumasi, Ghana, 02 December 2020.

Maelezo ya picha,

Rallies were held in recent days despite coronavirus restrictions

Vyama vikuu vya kisiasa vimepambana kwenye Twitter na Facebook kwa kutuma ujumbe wa kukinzana

Redio, televisheni na ujumbe mfupi wa maandishi pia vimetumika kufanya kampeni.

Hatahivyo, katika siku za mwisho za kampeni, tahadhari ilitupiliwa mbali wakati wanasiasa walipokutana na umati wa wapiga kura. Sasa kuna wasiwasi kuwa kunaweza kuwa na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.

Ghana imeripoti zaidi ya maambukizo 50,000 ya Covid-19, na watu wasiopungua 300 wanakabiliwa na virusi.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *