img

Tetesi za soka kimataifa

December 7, 2020

 

Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 27, amepata ofa na timu kubwa sita za ligi ya Primia-Manchester United, Liverpool, Chelsea, Tottenham, Manchester City na Arsenal. (90Min)

Manchester United inamfuatilia mlinzi wa Kiingereza wa Atletico Madrid Kieran Trippier, 30, huku Ole Gunnar Solskjaer akimuhitaji pia kwa ajili ya kumpa changamoto Aaron Wan-Bissaka, 23.(Telegraph)

Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 32, anaamini kuwa ataweza kupata klabu nyingine bora – lakini ana uwezekano wa kuondoka kabla ya msimu ujao. (Kioo)

Manchester United imeibuka kuwa kinara katika kinyang’anyiro cha kupata saini ya kiungo wa kati wa Argentina Thiago Almada, 19, wa Velez Sarsfield. (Todo Fichajes, via Team Talk)

Kiungo wa kati wa Liverpool, Mholanzi Georgio Wijnaldum, 30, amedokeza kuwa anasubiri klabu ichukue hatua kuhusu kuongeza mkataba wake. (Mirror)

Arsenal inaweza kulazimika kuharakisha uhamisho wa Dominik Szoboszlai wakati wa dirisha la Januari baada ya habari kuibuka kuwa Real Madrid wamepanga kutoa kitita cha fedha kwa ajili ya kiungo wa kati wa Hungary anayekipiga Salzburg. (Express)

Wadhamini wa shati wa Manchester United Chevrolet wanaamini itakuwa jambo la thamani kibiashara kusaidia kufadhili hatua ya kumrejesha, Old Trafford mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 35.(Auto Esporte, via Sun)

Mkurugenzi wa michezo wa Paris St-Germain Leonardo ameondoa matarajio ya klabu kumsajili kiungo mchezeshaji wa Argentina Lionel Messi ikiwa mchezaji huyo wa miaka 33 ataondoka Barcelona mwakani. (Mail)

West Ham ni miongoni mwa vilabu vingi vya England na Ureno vinavyomtolea macho mchezaji wa zamani wa Tottenham Marcus Edwards, winga wa Uingereza mwenye umri wa miaka 22 sasa anaichezea Vitoria Guimaraes. (Team Talk)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi anayekipiga katika klabu ya Brighton Dan Burn, 28, amesema wachezaji wa Albion watamuunga mkono mchezaji yeyote atakayebainisha kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja. (Argus)

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *