img

Songoro Mnyonge achaguliwa kuwa Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondon

December 7, 2020

 BARAZA la  Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, limemchagua  Songoro Mnyonge kuwa Meya wa  Halmashauri hiyo huku  Heri  Nassoro  kuwa Naibu Meya wa Manispaa hiyo.

Katika uchaguzi uliofanyika jijini Dar es Salaam, jana, Mnyonge ambaye ni Diwani wa Kata ya Mwananyamala  kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alipata kura  zote 29 zilizopigwa  sawa na silimia 100 huku Nassoro ambaye ni Diwani wa Kata ya Bunju (CCM) akipata kura 28.

Akitangaza matokeo hayo Mwenyekiti wa Muda  wa Uchaguzi  huo ambaye ni  Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni,   Stella Msofe, alisema  mgombea kwa nafasi ya  umeya alikuwa ni mmoja tu na kwa nafasi ya Naibu Meya alikuwa ni mmoja.

“Wajumbe walikuwa  walikuwa 29 ambapo kwa nafasi ya umeya  Mnyonge amepata kura 29. Hivyo ninamtangaza kuwa Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni,”alisema Stella.

Alisema kwa nafasi ya Naibu Meya, kura zilizopigwa ni 28 katika ya 29  kwani mjumbe mmoja hakupiga kura ya naibu meya.

“Hivyo ninamtangaza Nassoro kuwa Naibu  Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni,”alibainisha  Stella.

Uchaguzi huo, ulianza kwa  Baraza la Madiwani kuapishwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi  Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kinondoni,  Franco   Kiswaga ambaye aliwataka madiwani hao  kuwajibika kwa mujibu wa kiapo.

“Mnajua maana ya kiapo, kuwa waadilifu kutenda kazi kwa utii, bila huba wa chuku  upendeleo wala kumuonea mtu yoyote, bila kuangalia rangi jinsia itikadi wala hali ya mtu,”alisema Hakimu huyo.

Baada ya kiapo hicho, pia madiwani hao walikula kiapo cha Ahadi ya Uadirifu kwa Viongozi wa Umma, ambappo waliongozwa na  Ofisa Maadili Hamadi Bakari.

“Tamko hili ni baya  na la wazi  kwa kiongozi kuahidi atakuwa mwadirifu katika utekelezaji wa majukumu yake pamoja na kupambana na kampeni  dhidi ya rushwa,”alisema.

 Alisema , itazingatiwa kuwa, Desemba 9 mwaka huu ni Siku ya Duniani  lakini kwa hapa Tanzania itafanyika Disemba 10 kutokana na Disemba 9 kuwa Siku ya Uhuru wa Tanzania Bara.

“Kauli mbiu  ya mwaka huu katika maadhimisho hayo ni Uzingatiaji wa ahadi ya uadirifu   kwa viongozi na watumishi wa umma kwa ustawi na utawala bora na haki za binadamu,”alisema.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa, Meya Mnyonge, alisema atafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na madiwani akitumia falsafa ya  mipango shirikishi.

Alisema, ahadi  zilizo  changia  madiwani wote wa baraza hilo kutokana na CCM  ni utekelezaji wa ahadi na hivyo kuwataka madiwani kutimiza ahadi kwa vitendo.

“Lakini tushirikiane na mkurugenzi na watendaji kuhakikisha tunatekeleza Ilani kwa vitendo bila ubabaishaji. Manijua jina langu naitwa Mnyonge ila ni jina tu lakini katika utekelezaji sina  mchezo na  ernest mtu,”alisema Mnyonge.

Naye Naibu Meya, Nassoro, alisema, yuko tayari  kumshauri Meya, kushirikiana na madiwani na watendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha  halmashauri hiyo inasonga mbele.

Meya Mstaafu wa Baraza hilo, Benjamin Sitta, aliaga kwa kuwataka madiwani kutekeleza ahadi na kuwa na ahadi chache zinazo tekelezeka kuliko kuwa na ahadi nyingi kwa wananchi ambazo  haziwezi kutekelezeka kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, imemchagua Ernest Mafimbo kuwa Meya wa  Manispaa hiyo.

Meya huyo anatokana na CCM  na alichaguliwa kwa kura zote 13  zilizo pigwa  ukiwa ni ushindi wa asilimia 100.

Pia baraza  limemchagua  Stephano Warioba, kuwa Naibu Meya (CCM) ambapo pia alipata kura zote 19 zilizopigwa  sawa na asilimia 100.

Wagombea hao   hawa kuwa na mpizani katika kuwania nafasi hizo.

Manispaa hizo zinakuwa za awali kuchagua mameya katika mkoa wa Dar es Salaam, yenye manispaa sita ambazo ni Temeke, Kigamboni, Ilala, Ubungo na Kigamboni.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *