img

Selemani Nampanye Mwenyeki Mpya Halmashuri ya Wiaya ya Mtwara

December 7, 2020

Na Faruku Ngonyani , Mtwara

Diwani Mteule wa kata ya Mahurunga Selemani Ally Nampanye (Ccm) Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mkoani amechaguliwa kuwa Mwenyeki wa Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo kwa kupata kura 17 kati 29 zilizipigwa na wajumbe na Abduli Mahupa Diwani Mteule wa katai ya Ndumbwe (Cuf) akishika nafsi ya pili kwa kupata kura 11 huku kura moja ikiharibika.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imechuliwa na Abdalla Makame Diwani wa mteule wa kata ya Ziwani (Ccm) kwa kupata kura 18 kati ya 29 zilizopigwa na wajumbe na nafasi ya pili ilishikwa na  na Patrick Simwinga Diwani wa kata ya Tangazo(Chedema) aliyepata kura 11.

Mara baada ya kushinda kiti hiko cha Mwenyekiti wa Halmashauri Nampanye ameahidi kuonyesha ushirikiano kwa madiwani na wafanyakazi wote Halmashauri kuleta maendeleo kwa wanachi.

Jumla wajumbe halai 29 waliopiga kura kuwachagua Mwenyekiti na makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Mtwara huku kwa upande wa Mwenyekiti kura moja ikiharibika.

Awali  Madiwano hao wateule walikula kiapo cha utii cha kuwatumika wananchi na kuitumika Halmashauri hiyo kwa miaka mitano ijayo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *