img

Rais wa Zanzibar Dkt.Hussein Mwinyi amteua Seif Sharif Hamad kuwa Makamu wa kwanza wa Rais visiwani Zanzibar

December 7, 2020

Dakika 4 zilizopita

Kiongozi mkuu wa chama cha upinzani ACT Wazalendo Seif Sharif Hamad

Rais wa Zanzibar Dkt.Hussein Mwinyi amemteua Mwenyekiti wa chama cha upinzani ACT- Wazalendo Seif Sharif Hamad kuwa Makamu wa kwanza wa Rais visiwani humo.

Awali chama hicho kikuu cha upinzani kilikataa kuyatambua matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa kusema kwamba yalikua batili, hata hivyo chama hicho kimeongeza kwamba baada ya majadiliano ya muda mrefu pamoja na kupokea maoni ya wanachama wake, kimeamua kuungana na serikali ya chama tawala kwa ajili ya kuendesha nchi.

Awali akitangaza uamuzi wa kuungana na serikali ya CCM, Katibu Mkuu wa Chama hicho ADO Shaibu alisema uamuzi huo umeridhiwa na kamati kuu ya chama hicho baada ya kutafakari kwa kina. Shaibu alisema uamuzi huo sasa pia utawawezesha Madiwani, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge kupitia chama hicho, kuweza kushiriki kwenye vyombo vyao vya uwakilishi ili kuendeleza mapambano.

Katika mkutano maalum wa kamati kuu ya chama cha ACT Wazalendo, wameamua kuwa wapendekeze jina la mwanachama atakayekuwa makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar.

Pia ACT Wazalendo, imewaruhusu wajumbe wa baraza la wawakilishi, wabunge, na madiwani waliochaguliwa kukiwakilisha chama na wananchi waliowachagua.

Miongoni mwa sababu walizotoa kufikia uamuzi huo ni pamoja na kutathmini historia ya mapambano ya demokrasia Zanzibar na Tanzania bara kwa ujumla na kusema kuwa mara nyingi matukio ya raia kujeruhiwa, uwepo wa uhasama wa kisiasa, kudhalilishwa kijinsia na mali za watu kuharibiwa yamekuwa yakijirudia huku jambo muhimu ni kuwa na amani.

Aidha, Kamati kuu ya ACT, imeahidi kufanya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi Zanzibar ili kurejesha imani ya wananchi juu ya uwepo wa uchaguzi huru na wa haki.

Kwa mujibu wa Chama cha ACT Wazalendo, hali ilivyo kwa sasa Zanzibar inahitaji busara kubwa katika kuponya majeraha yaliyotokana na uchaguzi huo, ili kuhakikisha kuwa matukio ya namna hiyo hayajirudii tena.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *