img

Pompeo aukosoa uchaguzi wa Venezuela

December 7, 2020

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Mike Pompeo hapo jana ameukosoa uchaguzi wa bunge nchini Venezuela na kuuita uliojaa ulaghai na udanganyifu, vilivyochochewa na rais Nicholas Maduro.

 Uchaguzi huo ulioshindaniwa na wagombea 14,000 kutoka vyama zaidi ya 100 unafanyika wakati taifa hilo likiwa katikati ya mzozo mbaya kabisa wa mfumuko mkubwa wa bei, ukosefu wa maji na nishati ya gesi na kukatwa ghafla kwa umeme. 

Ushindi wa Maduro utakipatia chama chake cha Kisoshalisti viti 227 kwenye bunge la kitaifa, taasisi pekee ambayo haiko chini ya udhibiti wake, lakini pia utamuongezea nguvu na kumdhoofisha zaidi mpinzani wake anayeungwa mkono na Marekani, Juan Guaido anayeongoza kuususia uchaguzi akisema ni wa kilaghai.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *