img

Marekani, China zaendelea kudhibiti soko la silaha

December 7, 2020

Ripoti mpya ya taasisi ya kimataifa ya utafiti wa amani SIPRI yenye makao yake mjini Stockholm, SIPRI imeonyesha kuwa makampuni ya silaha ya China na Marekani yalilidhibiti soko la silaha ulimwenguni kwa mwaka 2019.

Ripoti mpya ya taasisi ya kimataifa ya utafiti wa amani SIPRI yenye makao yake mjini Stockholm, SIPRI imeonyesha kuwa makampuni ya silaha ya China na Marekani yalilidhibiti soko la silaha ulimwenguni kwa mwaka 2019. Lakini pia ripoti hiyo imesema Mashariki ya Kati kwa mara ya kwanza imeingia kwenye orodha ya wazalishaji wakubwa zaidi 25 wa silaha ulimwenguni.

Kulingana na ripoti ya SIPRI, makampuni ya Marekani na China ndio yaliyolikamata soko la silaha kwa mwaka 2019, wakati Mashariki ya Kati ikijitokeza kwa mara ya kwanza miongoni mwa vigogo 25 wa kuzalisha silaha ulimwenguni.

data zilizochapishwa na SIPRI hii leo zimeonyesha makampuni ya silaha yaliyojikita nchini Marekani yalichukua nafasi tano za mwanzo mwaka jana, wakati kampuni ya Lockheed Martin, Boeing, Northrop Grumman, Raytheon na General Dyanamics yakifanya biashara ya dola bilioni 166 katika  mauzo jumla ya mwaka.

Kwa ujumla, makampuni 12 ya Marekani yamekuwa miongoni mwa makampuni hayo 25 makubwa zaidi yanayozalisha silaha, na kufanya asilimia 61 ya mauzo jumla ya silaha.

China imeibuka ya pili kwa kufanya asilimia 16 ya mauzo ya silaha mwaka jana. Makampuni manne ya China yanayozalisha silaha yamejitokeza miongoni mwa makampuni 25 ya juu, wakati matatu yakiwa kati ya yale kumi ya mwanzo.

Mauzo ya silaha ya makampuni hayo manne ya China yaliongezeka kwa asilimia 4.8 kwa mwaka 2019 dhidi ya dola 56.7 bilioni za 2018. Orodha ya makampuni hayo ni Aviation Industry Corporation of China(6); China Electronics Technology Group Corporation (8); China North Industries Group Corporation (9), na China South Industries Group Corporation (24).

Mtafiti mwandamizi wa SIPRI Nan Tian amesema kwenye taarifa yake kwamba makampuni ya China yananufaika zaidi na programu za maboresho za Jeshi la Ukombozi wa Watu.

Taasisi hiyo imeongeza kuwa kuna uwezekano wa kuwepo kwa makampuni mengine yenye uwezo unaojitosheleza kuorodheshwa miongoni mwa makampuni hayo 25 ya juu zaidi ulimwenguni, lakini haikuwezekana kuyaingiza kwenye orodha hiyo kutokana na kukosekana data sahihi na za mlinganisho.

Mashariki ya Kati yaingia kwenye “klabu”.

Kwa mara ya kwanza, wazalishaji wa silaha wa Mashariki ya Kati wamejikuta ndani ya 25 bora ulimwenguni.

Umoja wa Falme za Kiarabu kwa mara ya kwanza yaigia kwenye uzalishaji wa silaha kwa wingi duniani

Kampuni ya EDGE ya Umoja wa Falme za Kiarabu imeshika nafasi ya 22, na kufanya asilimia 1.3 ya mauzo jumla ya silaha miongoni mwa makampuni hayo 25 vinara.

Kulingana na mtafiti mwingine mwandamizi wa programu ya matumizi ya kijeshi na silaha kwenye taasisi hiyo Pieter Wezeman, kampuni hiyo iliakisi namna ambavyo mahitaji makubwa ya kitaifa ya bidhaa za kijeshi, lakini pia nia ya kuachana na utegemezi wa mataifa ya magharibi, yalivyochochea ukuaji wa makampuni ya silaha katika eneo la Mashariki ya Kati.

Aidha, kwa mara ya kwanza kampuni ya Ufaransa ya Dassault Aviation Group nayo imeingia kwenye oroodha hiyo ya makampuni 25 makubwa ya uzalishaji silaha. Kampuni hiyo ilichangia ongezeko kubwa katika mauzo ya silaha ya kila mwaka kwa asilimia 105.

Kwa pamoja, mauzo ya silaha na huduma za kijeshi za makampuni hayo 25 zilifanya kiasi cha dola bilioni 361 kwa mwaka 2019, ambacho ni ongezeko la asilimia 8.5 tofauti na mwaka 2018.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *