img

Mama awaua watoto wake watatu kwa kuwapa Maembe yenye Sumu

December 7, 2020

 

Na John Walter-Manyara

Mama mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Regina Daniel (24) mkazi wa Louxmanda Kijiji cha Bashnet  Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara, anatuhumiwa kuwauwa watoto wake watatu kwa kuwalisha maembe yenye sumu inayodaiwa ni ya Panya .

Tukio hilo la kusikitisha limetokea Desemba 5 mwaka huu ambapo mtuhumiwa aliyapaka sumu maembe mawili kisha kuwapatia watoto hao.

Leo Jumatatu  Desemba 7,2020 Kamanda wa Polisi mkoa wa  Manyara ACP Paul Kasabago amethibitisha kutokea kwa tukio ambapo amesema chanzo cha Mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia kati ya mama huyo na mume wake ambao umesababisha mke kuchoshwa na maisha hayo na kuamua kufanya tukio hilo kwa lengo la kumuokoa mume wake.

Kamanda amewataja watoto waliopoteza maisha ni Emmauel Agustino (7), Emiliana Agustino (4) na Elisha Agustino ambaye umri wake ni mwaka mmoja (1).

Kasabago ameeleza kuwa wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa kwa ajili ya kumfanyia mahojiano.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *