img

Maafisa wa polisi wajeruhiwa baada ya mashambulizi kwenye kituo cha polisi Ugiriki

December 7, 2020

Maafisa 5 wa polisi wameripotiwa kujeruhiwa katika mashambulizi yaliyotekelezwa kwenye kituo cha polisi kilichoko mji mkuu wa Athens, nchini Ugiriki.

Kituo hicho cha polisi kilichoko wilayani Kolonos,  kilishambuliwa kwa mawe na marungu hapo jana na kundi la watu 70-80 walioficha nyuso zao kwa vinyago.

Katika mashambulizi hayo, ambapo maafisa 5 wa polisi walijeruhiwa 1 wao akiwa katika hali mbaya, wanaharakati walifungua mabango na kutoa kaulimbiu kwa sababu ya kumbukumbu ya kifo cha Alexis Grigoropulos, ambaye aliuawa mnamo 2008 kwa kufyatuliwa risasi ya polisi.

Baada ya mashambulizi hayo, polisi wametangaza kupiga marufuku maandamano yote ambayo yalipangwa kufanyika mjini leo hii.

Ilielezwa kuwa vituo vya usafiri wa metro vya katikati ya mji vitafungwa, na vikosi vya usalama vitachukua hatua kali za kiusalama.

Grigoropulos mwenye umri wa miaka 15, alipigwa risasi na polisi waliokuwa wakishika doria katika wilaya ya Eksarhia mjini Athens mnamo 6 Desemba 2008.

Kifo cha Grigoropulos kilipelekea maandamano kufanyika kwa siku nyingi ambapo majengo mengi ya umma, benki na sehemu za kazi zilichomwa moto.

Afisa wa polisi Epaminondas Korkoneas ambaye alihusika na kifo cha Grigoropulos, alihukumiwa kifungo cha maisha mnamo 2010.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *