img

Idadi ya vifo vya raia yaongezeka Yemen

December 7, 2020

Idadi ya raia wanaopoteza maisha kutokana na vita vya ndani nchini Yemen inaendelea kuongezeka kila siku.

Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (UN) ilitangaza kuwa raia 139 waliuawa na kujeruhiwa katika miezi miwili iliyopita katika eneo la Hudayda kutokana mizozo iliyoongezeka.

Katika taarifa iliyotolewa na ofisi hiyo, ilisisitizwa kuwa pande zote zinazozozana zinapaswa kuacha mashambulizi dhidi ya raia ambayo yanakiuka sheria za kimataifa.

Hafi kufikia sasa tangu kuanza kwa vita vya ndani vya Yemen, raia 12,000, na jumla ya watu 112,000 wamepoteza maisha.

Miongoni mwa watu waliopoteza maisha kuna watoto 2,138.

Wakati huo huo, kamanda mwandamizi kutoka Baraza la Mpito la Kusini aliyekuwa akiungwa mkono na serikali ya Abu Dhabi, aliuawa katika mji wa Ebyen.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *