img

Ghana: Uchaguzi wa Urais na wabunge waanza

December 7, 2020

 

Raia wa Ghana wanafanya zoezi la upigaji kura leo Jumatatu kwenye uchaguzi mkuu wa Urais na Ubunge.

Milolongo mirefu ya watu imeonekana katika vituo mbalimbali vya kura baada ya vituo hivyo kufunguliwa saa moja asubuhi.Rais Nana Addo Akufo-Addo wa chama tawala cha NPP anakabiliana na Rais wa zamani John Dramani Mahama, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha NDC.

Hii ni mara ya tatu kwa Akufo-Addo na Mahama kushindana, huku kila mmoja akiwa amewahi kumshinda mwenzake angalau mara moja. 

Addo aliibuka mshindi mwaka 2016, naye Mahama akashinda mwaka 2012.Licha ya kuwepo wagombea 12 wanaowania urais wakiwemo wanawake wawili, ushindani unatajwa kuwa kati ya Akufo Addo na Mahama.Tume ya uchaguzi inatarajiwa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo baada ya saa 72 baada ya zoezi la kupiga kura.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *