img

Fahamu kisa cha baba aliyemuua mwanaye

December 7, 2020

Jeshi la polisi mkoani Ruvuma, linamtafuta mtu mmoja anaejulikana kwa jina la Zeno Ndonde, mkazi wa Mbinga mkoani humo kwa tuhuma za kumuua mtoto wake kwa kumkata na Nyengo ubavuni huku sababu ikiwa ni ugomvi wa kugombania shamba.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Simon Marwa Maigwa, amesema kuwa tukio hilo limetokea Novemba 30,2020, na kwamba mara baada ya kufanya tukio hilo alikimbilia kusikojulikana na kumtaka ajisalimishe kokote alipo kwani mkono wa sheria ni mrefu utamfikia.

Aidha Kamanda Maigwa, amesema kuwa katika kuelekea kipindi hiki cha kilimo ni vyema migogoro yote ya mashamba ipelekwe kwenye ngazi za sheria na siyo kujichukulia sheria mkononi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *