img

Covid 19: Wazee na Madaktari kupokea chanjo wa kwanza

December 7, 2020

Jopo la wataalam wa matibabu nchini Ujerumani linapendekeza kuwa wauguzi, madaktari na wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 80 kuwa wa kwanza kupokea chanjo ya Covid-19.Rasimu ya mapendekezo iliyotolewa leo Jumatatu, inaonyesha kuwa watu milioni 8.6 watakuwa wa kwanza kupokea chanjo hiyo.

 Idadi hiyo ni zaidi ya asilimia 10 ya waakazi wa Ujerumani.Rasimu hiyo yenye kurasa 62 inafafanua kuwa kando na watu hao waliotajwa, wengine ambao wako katika hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa virusi vya Corona pia watapokea chanjo hiyo.

Watu wengine wenye afya nzuri na ambao wako chini ya umri wa miaka 60, wakikadiriwa kuwa watu milioni 45 katika kundi hilo kati ya watu milioni 83, watakuwa wa mwisho kupokea chanjo hiyo. Waalimu wamewekwa katika kundi la nne, ilhali watu wenye nafasi muhimu za serikali na wanaofanya kazi madukani wakiwa katika kundi la tano.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *