img

Brexit: Matumaini ya kufikiwa makubaliano ya biashara bado yako

December 7, 2020

Msemaji wa Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema Uingereza itaendelea kujadiliana na Umoja wa Ulaya juu ya makubaliano ya kibiashara baada ya Brexit alimradi pande hizo mbili zina wakati wa kufanya hivyo.

Msemaji huyo amesema upo uwezekano wa makubaliano kufikiwa, huku lakini akiondoa uwezekano wa kuongeza muda wa mazungumzo hayo ambayo yako katika awamu ya mwisho.James Cleverly, ni waziri wa mambo ya nje wa Uingereza anayehusika na masuala ya ukanda wa Mashariki na kati na Afrika Kaskazini.Cleverly amesema “Hakika, makubaliano yanaweza kufikiwa. 

Usahihishaji wa maneno ni muhimu sana. Makubaliano yanaweza kufikiwa, kuna fursa ya kupatikana kwa makubaliano ambayo ni rafiki kwa Uingereza na hata pia Umoja wa Ulaya. 

Kitu ambacho tumejifunza katika mazungumzo haya, ni kuwa yanaweza kwenda hadi dakika ya mwisho. Lingekuwa jambo zuri iwapo makubaliano yangefikiwa mapema lakini sio ajabu kuwa huenda mwafaka ukapatikana dakika ya mwisho.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *