img

Biden kumteua Xavier Beccera kama waziri wa afya

December 7, 2020

Rais mteule wa Marekani Joe Biden anapanga kumteua mwanasheria mkuu wa jimbo la California Xavier Becerra kama waziri wa afya na huduma za matibabu.

Uteuzi wa Becerra mwenye umri wa miaka 62, ambaye pia alikuwa anatajwa kuwa chaguo la Mwanasheria Mkuu, unakuja wakati ambapo Biden anakabaliwa na shinikizo la kuchagua watu wa matabaka mbalimbali katika baraza lake la mawaziri.Becerra ataongoza mfumo wa afya wa Marekani ambao unaonekana kulemewa na idadi kubwa ya maambukizo ya ugonjwa wa Covid-19 ikiwemo vifo vilivyopindukia 2,000 katika siku za hivi karibuni.

Wakati huo huo, Rais Donald Trump amesema wakili wake Rudy Giuliani amekutikana na ugonjwa wa Covid-19.Kwa mujibu wa mashirika ya habari ya Marekani ya New York Times na ABC, Giuliani mwenye umri wa miaka 76 amelazwa katika hospitali moja mjini Washington.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *