img

Aliyezalishwa na baba yake aomba msaada

December 7, 2020

Binti wa miaka 17, aliyefanyiwa ukatili ndani ya familia yake na kukatisha ndoto zake baada ya  kubeba ujauzito, amewaomba watanzania na mashirika ya kutetea haki za wanawake na watoto kumsaidia ili aweze kuendelea na masomo.

Akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kutembelea kijiji cha Bulimba, wilayani Kishapu, Mkoa wa Shinyanga, anapoishi binti huyo,ambaye alikatisha masomo akiwa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Ukenyenge baada ya kudaiwa kupewa ujauzito na baba yake mzazi ambaye walikuwa wanaishi naye wawili kutokana na mama yake mzazi kufariki dunia mwaka 2016.

“Nilifanyiwa vitendo vya ukatili, nilijifungua kwa operesheni naombeni msaada kwa ajili ya kumlea mtoto wangu niliachishwa masomo nikiwa kidato cha tatu” amesema Joyce Samwel

 Kwa upande wake Katibu wa vituo vya taarifa na maarifa vilivyojengewa uwezo na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) wilayani humo  Peter Nestory, amesema masuala ya ukatili hatuwezi kuiachia serikali peke yake bali ni jukumu la jamii nzima kupambana tamaduni zinazowaumiza watoto wakike

Aidha Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba amesema matukio ya ukatili wa kijinsia katika kipindi cha Juni hadi Agosti 2020 ni 231 ikilinganishwa na mwaka 2019 kipindi kama hicho yalikuwa 151.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *