img

Waziri Mkuu Majaliwa ameiagiza SUMAJKT kumaliza Ujenzi Hospitali ya Uhuru Desemba 20, Mwaka huu

December 6, 2020

 

Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa ameliagiza shirika la uzalishaji mali la Jeshi la kujenga taifa SUMAJKT kuhakikisha ujenzi wa Hospitali ya Uhuru iliyopo Chamwino Mkoani Dodoma inakamilika ifikapo Desemba 20 mwaka huu.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa maagizo hayo leo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo ambapo amesema SUMAJKT wafanye kila jitihada kuhakikisha ndani ya mda huo ujenzi unakamilika.

” Nimesikia maelezo la mkandarasi kwamba mpaka tarehe 15 mtakuwa mmemaliza na mimi nawaongezea siku tano hadi kufika tarehe 20 hii kazi iwe imekwisha,

” Na siku hiyo nitakuja mimi mwenyewe nitakuja hapa tarehe 19 kuona mmeishia wapi ili nikatoe taarifa kwa mheshimiwa Rais tayari kwa kuja kuzinduliwa  tunataka hospitali hii ianze kutoa huduma mwaka huu” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Amesema Serikali itatoa fedha nyingine kiasi milioni 835 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe za mwaka huu na fedha hizo zitaelekezwa katika hospitali kukamilisha na kununua vifaa tiba vya hospitali hiyo.

“Na hizo fedha tulizozitenga zitatumika kumalizia ujenzi, ujenzi wa uzio (fensi) na barabara itakayounganisha na barabara kuu na nyingine Sasa itumike kununulia vifaa tiba” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Rajabu Mabele, amesema rasmi ujenzi huo ulianza Desemba 2019 na ulitarajiwa kumalizika Desemba 2020 na mpaka Sasa umekamilika kwa asilimia 97 ili kukamilika kwake.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge ametoa ombi kwa Waziri Mkuu kuongezewa watumishi kwani pindi hospitali hiyo ikianza kufanya kazi kutakuwa na upungufu wa wataalamu wa afya kwani mpaka Sasa kuna upungufu wa wataalamu hao.

” Yani kabla ya kuanza kufanya kazi kwa hospitali hii tayari kama Mkoa tunaupungufu wa wataalamu wa afya ikiwezekana waje watumishi hata kutoka mikoani waje kuongeza nguvu” amesema Dkt Mahenge.

Aidha ameeleza upungufu wa vifaa tiba kama MRI na CT Scan upungufu ni mkubwa, sambamba na hilo ameomba makazi kwa watumishi wa hospitali ya Benjamini Mkapa ambao wengi wao wanaishi Dodoma Mjini jambo ambalo ni hatari endapo itatokea dharura usiku.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *