img

Wananchi wa Kuwait waanza zoezi la upigaji kura kwenye uchaguzi wa bunge

December 6, 2020

Nchi ya Kuwait imeandaa uchaguzi wa bunge katika kipindi cha janga la corona  (Covid-19).

Zoezi la upigaji kura lilianza nyakati za asubuhi ili kubainisha wabunge 50 watakaochaguliwa kuwakilisha bunge la taifa la Kuwait. 

Katika uchaguzi huo ulioandaliwa kwa kuzingatia tahadhari za janga la corona, jumla ya wagombea 326 wakiwemo wanawake 28 wanashindana. 

Nchi hiyo imegawanywa katika maeneo bunge 5 ambapo jumla ya watu 567,694 walisajiliwa kama wapiga kura. 

Wapigaji kura watachagua wagombea kumi kutoka kila eneo bunge watakaowawakilisha bungeni.

Zoezi la upigaji kura lilitatarajiwa kuendelea mpaka saa 20:00.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *